Wadau tusiisahau ligi ya wanawake ( Serengeti Lite Women’s Premier League)

Feb 7, 2023
61
36
5
Wadau wengi hapa bongo wanapenda mpira wa miguu, wanafuatilia zaidi muenendo wa ligi kuu Tanzania bara hasa timu pendwa Simba na Yanga.

Lakini wasiwasi yangu kubwa ipo kwenye soka la wanawake ambalo linakuwa kwa kasi kubwa sana kutokana na ushindani kuzidi kuongezeka.

Hii inachangiwa na udhamini uliyowekwa na Serengeti Lite, licha ya kuwa hautoshi lakini pia Shirikisho la soka (TFF) linajitahidi kuibeba ligi hiyo.

Timu za wanawake kwa msimu huu zimejitahidi sana kushindana hasa zile zenye Ukwasi (Simba Queens, Yanga Princess, JKT Queens nk).

Lakini bado wadau wengi wamelipa kisogo soka la wanawake licha ya juhudi kubwa,naamini kuna watu hawajui ligi ya wanawake ina jumla ya timu ngapi wala nani anaongoza msimamo wa ligi na kwa alama ngapi.

Ni wakati sasa wa wadau na mashabiki kutoa SUPPORT yao, ili kuongeza motisha kwa vilabu na wadhamini kuwekeza huko.

Leo Simba Queens wamecheza dhidi ya Ceasiaa Queens na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, kwa ushindi huo wanasalia kileleni kwa alama 22 michezo 9.
20230214_175905.jpg