WAHUNI WA SOKA WAIANDAMA YANGA

Kriss

Mgeni
Nov 4, 2022
102
138
5
WAHUNI WA SOKA WAIANDAMA YANGA

Miaka miwili iliyopita niliwahi kuwasikia wachambuzi mbalimbali wakiisifu klabu ya Simba kwa mtazamo wa kimaendeleo, walidiriki kusema Simba imewaacha Yanga mbali sana, hii ni katika kulinganisha yale mabadiliko ya kiuendeshaji klabu, yaliyokuwa yakifanywa na klabu hiyo kwa mlengo wa Mo Dewji kuwa mbia,
Wengi wa wachambuzi walisifia mchakato huo huku wakithibitisha kuwa Mo Dewji ametimiza vigezo vya kuwa muwekezaji 'mbia', na mbali zaidi walithibitisha kuwa Mo ameshaweka Billioni 20.
Nakumbuka kila jambo linalofanywa na Simba, wachambuzi waliizodoa Yanga kwa kusema kuwa Simba imewaacha Yanga mbali.

Leo tukiyaangalia mafanikio ya Simba yaliyonadiwa mno na wachambuzi, na ukilinganisha na mafanikio ya Yanga iliyozodolewa, hakuna hata mchambuzi mmoja aliyenadi mafanikio hayo.
Shafie Dauda ndiye niliyemshuhudia akiipongeza Yanga kwa kufungua Chanel yake maalum, nami nampongeza kwa hilo.

Kuna jambo walio wengi hawakulijua ama kwa makusudi hawakulijali, yaani wakati Simba wanasifiwa kwa mabadiliko yao, hakuna hata mwanayanga mmoja aliyewabeza, pia hakukuwahi kutokea watu waliokuwa wakizodoa ama kijaribu kuharibu mifumo ya ubadilikaji wao, haikutokea kushutumu ama kufanya hila na hujuma dhidi ya Simba, haikutokea kuwarubuni wachezaji wa Simba ili wavurugikiwe,
kwa wanayanga waliona kuwa mafanikio ya Simba ni kioo cha kuifanya Yanga ifanye mabadiliko makubwa na yenye tija zaidi.

Leo Yanga ilipo na inapokwenda, ni dhahiri kuwa tayari ipo kwenye kasi kuelekea kwenye maendeleo makubwa na kuwa klabu ya aina yake ndani ya Afrika,
Tofauti ilivyokuwa kwa wanayanga, wapinzani wa Yanga wametengeneza kundi maalum la kupinga maendeleo ya Yanga, kuhujumu na kurubuni wachezaji ili kuivuruga timu ya Yanga.

Wapo wahuni wanaojipenyesha kwa viongozi wa juu wa soka hapa nchini, wanajipendekeza kwa kujenga urafiki ili wapate kinga, wahuni hao hutumika na wapinzani wa Yanga kupitia kofia ya wanahabari, kila siku hukutana ama kuwasiliana ili kubuni mambo mapya ya kuiandama Yanga, kwa kuthibitisha hilo, hebu chukulia maamuzi ya awali yaliyotolewa na kamati ya maadili na nidhamu ya TFF, kuhusiana na shauri la Fei Toto, wahuni wamecharuka na kuonesha kutofurahishwa kwao na maamuzi hayo.

Kwa andiko hili, tunawatahadharisha wahuni kuwa, Yanga ni klabu kongwe na ina watu wengi wa kila rika na matabaka yake, hivyo basi hujuma na kero wanazotufanyia wanayanga tunazijua, nasi wanayanga tunaangalia hatua za kisheria ili tukomeshe vitendo hivi.

Tuwapinge wahuni kwenye soka kwa nguvu zote, soka la kisasa linaendeshwa kidigitaly na kwa uwazi zaidi, hivyo hujuma za kipumbavu hazileti maendeleo bali hudumaza soka letu.
 
  • Like
Reactions: McRay and Lukac

McRay

Mgeni
Nov 4, 2022
185
131

Tunapigwa sana vita