Wapinzani Wa Yanga Wazuiwa Kutumia Uwanja Wao Yanga Ishindwe Yenyewe Tu Kimataifa

Hammy36

Administrator
Jan 17, 2023
56
54
5
Dar Es Salaam
JAMBO Hili linaweza kuwa habari njema kwa Yanga baada ya wapinzani wao kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Vital’O FC kuzuiwa kutumia uwanja wao wa nyumbani wa Intwali uliopo Bujumbura, Burundi.

Ukaguzi uliofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) umebaini kuwa uwanja huo wa Intwali hauna sifa za kutumika kwa mashindano ya klabu Afrika kuanzia hatua ya awali.

Katika orodha ya viwanja iliyotolewa na CAF, hakuna jina la Uwanja wa Intwali jambo linalozilazimisha timu za Burundi zitakazoshiriki mashindano ya CAF msimu ujao kucheza mechi zao za nyumbani nje ya nchi yao.

Huo ni muendelezo wa timu za Burundi kucheza mechi za kimataifa za nyumbani nje ya nchi hiyo ambapo msimu uliopita zilitumia viwanja vya Azam Complex na Benjamin Mkapa vilivyopo Dar es Salaam.

Viwanja viwili vimepitishwa kutumika na timu za Tanzania ambavyo ni Benjamin Mkapa na Azam Complex.

Hiyo inamaanisha kuwa Uhamiaji na JKU za Zanzibar zitacheza mechi zao za nyumbani Dar es Salaam.

Msimu uliopita Yanga ilikutana na bahati kama hiyo kwenye mechi yake ya raundi ya kwanza ambapo timu ya El Merrikh ya Sudan ilitumia Uwanja wa Pele uliopo Kigali, Rwanda kutokana na Caf kutoupitisha Uwanja wa Omdurman wa kwao Sudan kutokana na sababu za kiusalama.