YANGA HAWASHIKIKI.

kidudumtujr

Mgeni
Dec 14, 2022
50
70
5
Tanzania
Yanga yaikalisha Coastal Union

Magoli mawili yaliyofungwa na Fiston Mayele yameiwezesha Yanga kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC.

Mayele amefunga magoli hayo katika dakika za
39 na 48 na kufikisha magoli 13 msimu huu akiwa mfungaji bora mpaka sasa akifuatiwa na Moses Phiri mwenye magoli 10.

Goli lingine la Yanga lilifungwa na Feisal Salum dakika ya 66.

Yanga SC imeongeza wigo wa alama 7 kati yake na Simba SC iliyopo nafasi ya pili yenye mchezo mmoja mkononi.

Coastal Union inasalia nafasi ya 13 alama 15 baada ya mechi 17.FECD204D-838A-4532-A826-1F715D1AF86E.jpeg