Yanga ilijua cha kufanya dhidi ya TP Mazembe

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
Yanga ilijua cha kufanya dhidi ya TP Mazembe.

Kocha wa Yanga Prof. Nasreddine Nabi anastahili pongezi nyingi, first eleven yake ya mechi ya jana dhidi ya TP Mazembe, ilikuwa ni first eleven ambayo iko well balanced, na timu ilikuwa ikicheza kwa kuelewana sana, na kila mchezaji alifanya kazi yake ipasavyo,

Lakini si vibaya kusema kwamba Yahya Mudathir alikuwa ndio mwiba kwa TP Mazembe siku ya jana, aliwamudu sana akiwa anashambulia na akiwa anazuia, he was absolutely superb kwenye muda wote wa dakika 67 alizocheza.

Team spirit ilikuwa juu sana, bila shaka wakienda nayo hivi, wanaweza kumaliza hatua ya makundi vizuri hata kama sio kufuzu kwenye next stage.

A610766C-F9B5-43F7-B617-5C36B02C48BF.jpeg