Yanga SC vs Monastir Pointi tatu kwa Yanga zimewapeleka mpaka kileleni

jamal

Mgeni
Nov 4, 2022
148
90
5
Yanga SC wamecheza hii mechi kwa hesabu kubwa sana , katika vipindi vyote viwili wameonesha sura mbili tofauti : Jinsi gani ya kutawala mchezo na kushambulia na pia jinsi gani ya kuzuia na kufunga duka vizuri

Viungo watatu wa kati SureBoy Aucho na Bangala kipindi cha kwanza walitawala sana mchezo , Bangala kwenye namba 6 wakati Aucho na Sureboy walisogea juu kama namba 8 wawili kazi yao kubwa ku connect na mawinga mawili ili kucheza mipira nyuma ya fullbacks wa Monastir

Musonda na Moloko .. movements zao zilikuwa za aina mbili : Kupita nyuma ya fullbacks wa Monastir kama Djuma na Lomalisa hawajapanda na pia mara nyingine kushambulia katikati ya fullbacks na centrebacks wa Monastir kama Djuma na Lomalisa wamefanya overlaps

Wakati huo huo Aucho na Sureboy kazi yao ni kupokea zile rebounds ili kurejesha mashambulizi tena ( Sustain attacks )

Nafikiri Monstair ni kama walikuja kwa ajili ya sare , kipindi cha kwanza walikaa nyuma sana wakisubiri counter attacks ambazo zilishindikana kwasababu ya shape ya ulinzi ya Yanga ilikuwa nzuri pale walipokuwa na mpira ( rest defense )

Kipindi cha pili Yanga SC waliamua ku manage mechi tu , kuwaacha Monastir wakae na mpira wakiwa nyuma lakini wakivuka tu mstari wa kati Yanga wanapora haraka mpira na kuanzisha counter attacks kwa kutumia kasi ya Moloko Musonda na Mayele na pengine kama kungekuwa na ukatili zaidi basi ni zaidi ya 2-0 , Jinsi Musonda na Moloko walivyokuwa wanafanya uwanja kuwa mpana , kuwalazimisha mafullback wa Monastir kukabia pembeni zaidi na kufungua njia za pasi kwenda kwa Mayele

images (21).jpg