Yanga vs Polisi Tanzania

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
Yanga leo wanaenda kuanza Mzunguko wa pili wakiwaalika Polisi Tanzania kwenye uwanja wao wa nyumbani Benjamin Mkapa Dar es Salaam ni mzunguko wa pili Yanga akiwa kinara wa ligi hiyo ya NBC kwa pointi 38, huku Polisi Tanzania wakiwa nafasi ya 16 na pointi kwenye ligi 9

Mzunguko wa kwanza Yanga alipata ushindi wa goli 2-1 katika uwanja wa ugenini wa Polisi Tanzania akiibuka na pointi 3 muhimu, Mechi tano za mwisho Polisi Tanzania alizokutana na Yanga Amekua akichezea kichapo kwenye mechi 4 na kuambulia draw mechi moja tu dhahiri Yanga anezidi kumtawala Polisi kwa kila Idara kila wanapokutana iwe nyunbani iwe ugenini.

Leo tena wawili hawa wanakutana kwa mkapa midaa ya saa 01:00 usiku kuzisaka pointi tatu muhimu Yanga akienda kutetea ubingwa na nafasi yake kama kina wa ligi na Polisi Tanzania kujikwamua matatizoni kutoka katika nafasi za chini na kuzidi kujiweka nafasi za Juu kubaki kwenye ligi nani ataibuka na ushindi leo?