Yanga walistahili Alama tatu lakini hata hii mojan kimahesabu ni nzuri pia

Kriss

Mgeni
Nov 4, 2022
102
138
5
Yanga wamekuwa kwenye form nzuri sana wakicheza kwenye viwanja vya ugenini, japo sio kila mara wanapata matokeo ila uwezo wao wa kumiliki mpira na kucheza kwenye falsafa zao upo pale pale.

Msimu huu kwenye michuano ya kimataifa Yanga kacheza away mechi 4, Al Hilal, Club Africain, US Monastir na Real Bamako. Zote Walicheza vizuri na kutawala mchezo.

Game ya jana Yanga walipaswa kuondoka na alama zote 3, ila concentration ilipungua dakika za mwisho Wachezaji walikuwa ni kama wameshamaliza mechi kichwani..maana goli lililofungwa ni mazingira ambayo watu hawakuwa kwenye mchezo.

Kuumia kwa Khalid Aucho kulifanya pressing ya Yanga ianze katikati, kwani ilibidi Mudathir ashuke kucheza na Bangala ili Aziz Ki acheze namba 10, ndio maana baada ya Aucho kutoka Real Bamako walianza kuja kwa kasi golini kwetu uwepo wa Mudathir mbele ya viungo wakabaji na nyuma ya Mayele kunaifanya Yanga ianze kukabia juu na kuwapa advantage kwenye umiliki.

Yanga wanarudiana na Real Bamako hapa Dar, nadhani Mwalimu Nabi hataki kingine zaidi ya alama tatu kwenye huo mchezo, kwani inawezekana


1677492165865.png