Yanga wanazidi kunoa kikosi chao kwa kasi sana

Lukac

Mgeni
Nov 4, 2022
120
83
5
Timu ya Yanga wanaendelea kuachia vyuma kwenye hili dirisha dogo na kwa sasa tayari wameshatambulisha chuma kimoja "Yahya" na wapo njia kuangusha vyuma vingine viwili muda wowote kwanzia sasa, kwa namna wametoa taarifa hii ni kama inaleta mshtuko sana kwa namna ya kikosi chao kinavozidi kuimarika siku baada ya siku msimu baada ya msimu wanataka nini hawa??

Club ya Yanga mpaka sasa imeshamtambulisha kiungo Mudathir Yahya kama mchezaji wao wa kwanza kumsajili kwenye dirisha dogo na tulimwona alianz akukupiga uko Zananzibar kwenye Mapinduzi Cup, huku Kennedy akihusishwa kutua jangwani

Ujio wa wachezaji hao tu unaleta mtazamo tofauti kwenye kikosi cha Yanga na ukizingatia namna vilivyo bora. Ukuta ni balaa, Viungo wameshibana, Mbele kunatisha,

Hata namna kocha wa Yanga anavozungumzia timu inaonesha ni namna gani Yanga wanatengeneza malengo yao kwa usahihi "Bado hatujamaliza kazi katika kuboresha timu lakini nimefurahi kupatikana kwa Mudathir, huyu ni kiungo ambaye namjua ubora wake naamini naweza kuwa na mengio ya kueleza wakati ukifika hasa baada ya usajili kukamilika, kitu muhimu tunatka kuongeza watu bora ambao watakuja kuongeza ushindani wa nafasi," alisema Nabi.
Nyota wa zamani wa kimataifa wa Yanga na Taifa Stars aliyetamba pia na Tukuyu Stars, Sekilojo Chambua alisema amekoshwa na ujio wa Mudathir katika kikso chao kwa kuwa uwezo wake unajulikana lakini pia anaona zitakuwa habari njema kama Yanga itamalizana na Musonda.
"Sina uhakika sana juu ya taarifa za Musonda lakini niseme kama atasajiliwa mshambuliaji hizo zitakuwa taarifa njema kwa kuwa tuna uhitaji wa mshambuliaji mwingine ambaye atakuja kuongeza nguvu katika mashindano ambayo tunacheza,"alisema Chambua.
"Tumeona usajili wa Mudathir sote tunamjua kwamba ni kiungo mzuri ana uwezo mkubwa wa kukaba na hata kushambulia, ujio wake ndani ya Yanga utaongeza kitu kikosini," ni Maneno Nabi.