Young Africans yaweka historia kwa kucheza mechi 49 bila kufungwa

Kriss

Mgeni
Nov 4, 2022
102
138
5
Timu ya Ligi Kuu ya Tanzania, Young Africans Sports Club imeandika historia katika soka la Afrika kwa kuwa miongoni mwa timu tano bora barani humo kushikilia msururu mrefu wa Ligi bila kufungwa.
Ikisimamiwa na Nasreddine Nabi wa Tunisia, Young Africans SC imekuwa timu inayoongoza Tanzania kushikilia msururu mrefu zaidi wa kutokufungwa kwenye Ligi na nafasi ya 4 barani Afrika.

Young Africans waliandika historia hii siku chache zilizopita walipoichapa Mbeya City mabao 2-0, lakini hawakufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 50 baada ya kufungwa 2-1 ugenini na Ihefu FC Jumanne Novemba 29, 2022 jijini Mbeya.

Mara ya mwisho Young Africans kupoteza mechi ilikuwa Aprili 25, 2021. Msimu uliopita Young Africans ilishinda mataji matatu nchini Tanzania na pia imefuzu hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF la TotalEnergies 2022/2023.

Eng. Hersi Said, Rais wa Young Africans SC aliweka wazi kuwa kama Klabu wanafuraha kuvunja rekodi katika soka la Tanzania ya kutofungwa kwa muda mrefu kwenye Ligi. "Tunafuraha kuhusu rekodi hii na pia kuwa miongoni mwa rekodi bora barani Afrika," aliongeza Said.

Ingawa Young Africans SC ilipokea kichapo cha mabao 2-1 ugenini kutoka kwa Ihefu Jumanne, bado wanasalia kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na pointi 32 katika mechi 13 ilizocheza.

Azam FC ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi sawa wamecheza mechi moja zaidi, huku Simba SC wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 31 za mechi 14 ilizocheza.

ASEC Mimosas inashikilia msururu mrefu zaidi wa kutopoteza Afrika katika mechi 108, huku Esperance de Tunis (Tunisia) ikishika nafasi ya pili kwa mechi 85, huku timu ya jeshi la Rwanda APR ikishika nafasi ya tatu kwa mechi 50.

Young Africans SC sasa wameingia katika nafasi ya nne, huku vigogo wa Afrika, Al Ahly kutoka Misri wakishika nafasi ya tano wakiwa na mechi 46.
Young Africans yaweka historia kwa kucheza mechi 49 bila kufungwa.
571bd592-5e81-4041-a3da-aff7df20b2f0.jpg
 
  • Like
Reactions: Nabi