Ahoua Jean Charles usajili bora zaidi Tanzania

Bakari

Mgeni
May 27, 2024
27
31
5
Sio sababu ni MVP Ivory Coast pekee. Hapana. Hadi sasa tumeshuhudia wachezaji bora Ivory Coast wanatua katika ardhi Yetu. Aziz Ki na Pacome huwezi acha kuwataja - moja ya sajili bora kabisa katika ardhi zetu.

Hakuna anayepinga Aziz Ki na Pacome ni wachezaji bora katika league yetu. Sasa jaribu kufikiri huu ubora waliokua nao wangekua ni chini ya miaka 23 au hata 25? Sidhani kama ingekuwa ni rahisi kuwapata au kuwalinda katika league yetu. Lakini hao niliowataja tunaweza kuwapata au kuwalinda sababu tayari ni jioni. Jioni kwa maana ya kuwa ukiwa above 26 ni ngumu sana kucheza nje ya Africa.

Pia tunakubaliana kuwa West Africa ndio feeder wazuri wa League 2 -League 1 (France) pia kidogo North Africa. Hivyo basi wachezaji wadogo wengi wenye vipaji vikubwa huwa tunategemea basi safari yao ni League 2 au wameshindwa sana basi ni North Africa.

Leo Simba inaenda kumtambulisha MVP wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 22 katika ardhi ya Tanzania. Hili sio jambo dogo hata kidogo. Wengi watachukua jambo la kawaida, ila kiuhalisia ni jambo kubwa sana.

Wengi watasema labda ni garasa, hajui mpira. Nitaomba huyo mtu anitajie ni mwaka gani League 1- Ivory Coast ilizalisha MVP mwenye kiwango cha kawaida? Tofauti, na nchi nyingine, ile league haina ushindani kama maana ubora katika ramani ya soka Africa, ila ni ardhi yenye vipaji vikubwa sana.

Kufuatia kile nilichokieleza basi bila kigugumizi, natamka kuwa huu ndio usajili bora kwa Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.
 
Wistabby

Mgeni
Jun 22, 2024
20
2
5
Naona Simba sasa imeamua kujenga timu yake Wana kijiwenii. kutokana na usajili wa mahitaji Simba Kila sehemu ya kikosi wamegusa kwa asilimia kubwa binafsi nategemea kuiona mbali
#nguvumoja
 
Eddy de Jr

Mgeni
May 9, 2024
91
16
5
Tusisahau kuna mwamba mmoja anaitwa AUBIN KRAMO,,,,mwenyezi Mungu naomba umjalie uponaji huyu mwamba wetu. Hakika Simba SC naiona ikiwa bingwa wa CAF Confederation Cup 2024/2025.
 
mrumi

Mpiga Chabo
Jul 4, 2024
5
1
0
Sio sababu ni MVP Ivory Coast pekee. Hapana. Hadi sasa tumeshuhudia wachezaji bora Ivory Coast wanatua katika ardhi Yetu. Aziz Ki na Pacome huwezi acha kuwataja - moja ya sajili bora kabisa katika ardhi zetu.

Hakuna anayepinga Aziz Ki na Pacome ni wachezaji bora katika league yetu. Sasa jaribu kufikiri huu ubora waliokua nao wangekua ni chini ya miaka 23 au hata 25? Sidhani kama ingekuwa ni rahisi kuwapata au kuwalinda katika league yetu. Lakini hao niliowataja tunaweza kuwapata au kuwalinda sababu tayari ni jioni. Jioni kwa maana ya kuwa ukiwa above 26 ni ngumu sana kucheza nje ya Africa.

Pia tunakubaliana kuwa West Africa ndio feeder wazuri wa League 2 -League 1 (France) pia kidogo North Africa. Hivyo basi wachezaji wadogo wengi wenye vipaji vikubwa huwa tunategemea basi safari yao ni League 2 au wameshindwa sana basi ni North Africa.

Leo Simba inaenda kumtambulisha MVP wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 22 katika ardhi ya Tanzania. Hili sio jambo dogo hata kidogo. Wengi watachukua jambo la kawaida, ila kiuhalisia ni jambo kubwa sana.

Wengi watasema labda ni garasa, hajui mpira. Nitaomba huyo mtu anitajie ni mwaka gani League 1- Ivory Coast ilizalisha MVP mwenye kiwango cha kawaida? Tofauti, na nchi nyingine, ile league haina ushindani kama maana ubora katika ramani ya soka Africa, ila ni ardhi yenye vipaji vikubwa sana.

Kufuatia kile nilichokieleza basi bila kigugumizi, natamka kuwa huu ndio usajili bora kwa Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.
Apewe muda tu anawez kuonyesha mengi mazuri. Asipopewa muda haya yote yatakuwaa story tu..