ARSENAL YAPIGWA 2-1 PALE PALE EMIRATES
WENYEJI, Arsenal wamechapwa 2-1 na Brighton & Hove Albion kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya Brighton leo yamefungwa na Leandro Trossard dakika ya 28 na kiungo Mzambia, Enock Mwepu dakika ya 66, wakati la Arsenal limefungwa na Martin Odegaard dakika ya 89.
Kwa ushindi huo, 37 katika mchezo wa 31 ikisogea nafasi ya 11, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 54 za mechi 30 nafasi ya tano.