
Ligi hiyo ilisimama kupisha michuano ya kombe la Dunia iliyomalizika Qatar.
Kocha huyo amewaambia wachezaji wake kuwa kama wanataka kushinda taji msimu huu, basi wacheze kwa kujituma kama ilivyokuwa kabla ya ligi hiyo kusimama.
Arsenal, iliyoshinda taji la mwisho la ligi mwaka 2004 , ilianza vema msimu huu kwa kushinda mechi 12 kati ya 14 ilizocheza.
Hata hivyo, Arsenal tayari itamkosa Gabriel Jesus katika mechi zake za awali baada ya mchezaji huyo kuumia katika michuano ya kombe la Dunia akiwa na Brazil.
Licha ya kumkosa Jesus, Arteta amekuwa na matumaini ya kurejea vema katika ligi, akijiandaa na mechi ya Jumatatu dhidi ya West Ham.
Newcastle United, ambayo ipo nafasi ya tatu katika msimamo nao watakuwa uwanjani Jumatatu dhidi ya Leicester.
" Napenda tucheze kwa kujituma kama ilivyokuwa awali ili tushinde taji msimu huu," amesema.
Arsenal imezidiwa pointi 5 tu na Manchester City wanaoongoza ligi.
City pia watakuwa uwanjani siku ya Jumatano ikivaana na Leeds.