Barbara Arudi Simba?

DeviMitupio

Mgeni
May 27, 2024
9
4
5
Uongozi wa Simba upo kwenye mabadiliko ya ndani ambapo nafasi zinazohusishwa sana, ni nafasi ya CEO Iman Kajula ambaye amekubali kujiuzulu kwenye nafasi hiyo, pamoja na nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi inayokaliwa na Salim Try Again.

Kuna mabadiliko kadhaa ambayo tayari yamefanyika ndani ya Simba, tena kwa siri kubwa ambapo Crescentius Magori na Swedy Nkwambi wamerudishwa na kupewa nafasi ya kusimamia kamati ya usajili wa timu hiyo.

hapo awali, Barbara aligoma kurudi Simba mpaka pale baadhi ya watu aliowataja kuwa hahitaji kufanya nao kazi, watakapoondoka ndiyo atarudi.

Kwa habari hizi ina maanisha kwamba, Barbara Gonzalez alichokitaka kimetimizwa na yupo huru kufanya kazi ndani ya miamba hiyo ya soka Tanzania na Afrika.

Enzi za utawala wake kabla hajatangaza kuachia kiti chake cha Ukurugenzi, Barbara Gonzalez alifanikiwa kwa kiasi chake kuipambania Simba ndani na nje ya Tanzania.

Mafanikio yake yalikuwa ni kutetea ubingwa wao kwa msimu wa 2020/21, Kuchukua kombe la Shirikisho na kufanya sajili bora kulinganisha na miaka ambayo yeye aliondoka.

Moja ya sababu iliyomuondoa Simba kipindi hicho, inaelezwa ni fitina za baadhi ya Viongozi na watu aliokuwa anafanya nao kazi, kitu kilichomfanya kushindwa kuvumilia na kujiuzulu nafasi yake.
 
KakaMkubwa

Mgeni
May 27, 2024
8
1

Babra alikuwa kiongozi mzuri Simba, itakuwa walimzingua kweli na aliona haya majanga yanayotokea saivi nahisi ndo sababu kubwa kujiuzuru. labda akirudi Simba itakuwa kama zamani.