Bomu limepiga tik tok tik tok mara kabum Jang'ombe (Mudathir Yahya)

McRay

Mgeni
Nov 4, 2022
185
131
5
Naambiwa l Mudhathir hajacheza miezi 6

Vipi kuhusu fitness yake?
Kiwango chake kiko katika hali gani?
Tumemsajili kwa ‘reference’ ya miezi 6 nyuma?

Natamani kujua
Sio kucheza, hana timu kwa miezi 6 ila na amini alikuwa anafanya mazoezi
Kipengele cha fitness tumuachie Mtunisi atadeal naye atanyooka na kufika fitness levels inayotakiwa
 

kamakawa

Mgeni
Nov 4, 2022
60
57
5
Kwanini Mauya mnachukulia poa sana
Misimu miwili nyuma alikuwa roho safu yetu ya kiwango yeye na Mukoko
Sijui kwa nini watu wanamchukulia poa Mauya, ila kuna muda naelewa Uhuru wa maoni.

Mauya alikuwa kiungo bora wa Ligi yetu Msimu mmoja kabla ya kutua Yanga, lakini Msimu wa kwanza alipotua Yanga akawa mchezaji muhimu sana leo wakina Aucho wametusahaulisha kabisa umuhimu wa Mauya.
 

Zawadi

Mgeni
Nov 4, 2022
41
17
5
Kwanini Mauya mnachukulia poa sana
Misimu miwili nyuma alikuwa roho safu yetu ya kiwango yeye na Mukoko
Mauya ni type ya Himid Mao.

Watu uwa wanamchukulia poa jamaa akiwa Taifa stars ila mimi uwa namuelewa sana.

Mauya anajua boli sema ni vile Yanga tunao viungi wengi na wazuri sana hvo tunamchukulia poa jamaa.