CHELSEA

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

CHELSEA YAILIMA SPURS 2-0 DARAJANI.​

AVvXsEiRd5j8ShnPrBcRzSo8BnqO7JxT-3E6bbjNFAuaZdflIlCKTWrHoMjgVBRxHXBPMpX1IaEtCJl7uaewgZiGEEw2dgkgtQKZcANNABuKzCO2ecmYlM2wOR9R8lEOFr364OeJDGCuFC0MXHDnr3wGE0OJWK5m4PxkOiO4EeBGEUhcD1n5YVVdDeNPc3G6=w640-h458

MABAO ya Hakim Ziyech dakika ya 47 na Thiago Silva dakika ya 55, yameipa Chelsea ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku was Jumapili Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Chelsea inafikisha pointi 47 katika mchezo wa 24, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na Liverpool ambayo pia ina mechi mbili mkononi, wakati Spurs inabaki na pointi zake 36 za mechi 20 katika nafasi ya saba.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Klabu za Liverpool pamoja na Brighton zimetoa malalamiko yao kwa Bodi ya Premier League kuhusu vyumba vya kubadilisha nguo vya uwanja wa Chelsea (Stamford Bridge)
Malalamiko yaliyotolewa ni:
☑️
Udogo wa chumba cha kubadilishia nguo
☑️
Ukosefu wa hewa ya kutosha kwenye chumba hicho
☑️
Hakuna mgawanyo wa bafu za kike na kiume (kutokana na uwepo wa wafanyakazi wao wa kike wanaosafiri na timu kuwa na wakati mgumu wanapofika uwanjani hapo)
Premier League tayari wametoa maagizo kwa Chelsea kuhakikisha wanarekebisha jambo hilo kwa wakati.
Inaweza kuwa picha ya ndani
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Beki wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger
🇩🇪
anaendelea kula likizo yake huko Sierra Leone
🇸🇱

Huu ni zaidi ya upendo kutoka kwa watu wa nchi hiyo.
Inaweza kuwa picha ya Watu 2, watu wanasimama na nje
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Baada ya kumaliza Mapumziko yake nchini Sierra Leone Antonio Rudiger ameondoka nchini humo na kurejea England kwa usafiri wa ndege binafsi.
Image
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Mchezaji wa Chelsea, Hakim Ziyech ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa Morocco
🇲🇦
leo akiwa na miaka 28.
Amecheza mechi 40 na kufunga 17.
Ziyech quits Morocco national team after AFCON snub - Vanguard News
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LUKAKU AIPELEKA CHELSEA FAINALI KOMBE LA DUNY.​

AVvXsEjF0vvoS_qvp7pWzfsmHTPt12WPyM50jpwabqpTK4-63OrsHfqg8Wy9H1_xAJA9R04xusPDPh6UE-pU4-n5_34MxhQ9nknsq0Tq06LiQl66pdPCoR7kE-Jc1YFQtHR2Zd6g4EW76JrDyg5txaNUW-NT9tjriFRsAhdGn7LRioB_icVU2QQlfClH_DAj=w640-h470

BAO pekee la mshambuliaji Mbelgiji, Romelu Lukaku dakika ya 32 limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Al Hilal katika mchezo wa Nusu Fainali Klabu Bingwa ya Dunia usiku wa Jumatano Uwanja wa Mohammed Bin Zayed Jijini Abu Dhabi, Saudia Arabia.
Sasa mabingwa hao wa Ulaya watamenyana na Palmeiras ya Brazil katika Fainali Jumamosi baada ya Mabingwa hao wa Amerika Kusini kuitoa Al Ahly ya Misri.
Kwa upande wao, mabingwa wa Asia, Al Hilal watawania nafasi ya tatu dhidi ya mabingwa wa Afrika, Al Ahly Jumamosi pia.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

CHELSEA YAICHAPA CRYSTAL PALACE 1-0​

AVvXsEjRs3AoOSkqCTwIr6gPWfqOE_7epaN1fY9KfE4-FJSRNxAdbAuaqfCAH4AMVbN6y-6oKD3hHz24IBanjPYpg3yxZlrL6evMwkiybJY9Vv6dLMcWQOnApJ695wKPqhvHrd869qFYdRwZwEW5yxbcWboVm-aoZLfqvwoNaUkqSGEI2ojDQbTyr3iS2h5e=w640-h444
BAO pekee la Hakim Ziyech dakika 89 limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
Chelsea inafikisha pointi 50, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi mbili na Liverpool baada ya timu zote kucheza mechi 25, wakati Palace inabaki na pointi zake 26 katika nafasi ya 13.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Tuchel amtetea Kepa​

Kepa PIC


LONDON ENGLAND. KOCHA wa Chelsea, Thomas Tuchel ametetea uamuzi wa kumwingiza kipa Kepa Arrizabalaga makusudi kwa ajili ya tukio la kupigiana penalti kwenye fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool uwanjani Wembley juzi Jumapili.
Baada ya dakika 120 bila ya bao, pambano hilo la kibabe lililazimika kuingia kwenye tukio la kupigiana penalti, ndipo Kepa, ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Edouardo Mendy, kushindwa kudaka mkwaju wowote, hadi hapo na yeye alipokuja kukosa wa kwake, akiiponza Chelsea kubeba ubingwa huo mara tisa, ikiibwaga The Blues kwa penalti 11-10.
Kepa, aliitumia Chelsea katika kila dakika ya kombe hilo hadi hapo fainali, alipompisha Mendy na baadaye kuingizwa dakika chache kabla ya tukio la kupigiana penalti. Mechi hiyo ilikuwa ya kibabe kwelikweli, mabao manne yakikataliwa na VAR.
Kocha Tuchel alisema: “Tunajisikia vibaya sana kwa ajili yake. Inauma kwamba ni yeye pekee ndiye aliyekosa penalti, lakini hatumlaumu. Nimefanya maamuzi niliyofanya, siwezi kutoa hukumu kwa sababu nafahamu kilichotokea. Hatujui kingetokea nini kama tungemwaacha Edou golini. Hatumlaumu Kepa. Lawama zote nipewe mimi, ndiye niliyefanya uamuzi. Wakati mwingine haya mambo yanatiki, wakati mwingine yanagoma. Hivyo ndivyo yalivyo maisha ya makocha kwenye soka.”
Tuchel alitumia mbinu zilezile alizotumia kwenye fainali ya European Super Cup, Agosti mwaka jana, ambapo Kepa aliingia uwanjani kuisaidia Chelsea kuichapa Villarreal na alisema: ìLazima tukibali viwango vya wapinzani wetu. Liverpool ni moja ya timu hatari sana kwa kushambulia Ulaya. Kukaba kule tulikokaba, kucheza kule tulikocheza, nimefarijika. Hatuna tunachojutia.î
Liverpool wao wamenasa taji la kwanza kati ya nne wanayoshindania msimu huu.
Kipindi cha kwanza kilikuwa cha kibabe kama ilivyokuwa kwenye kipindi cha pili na kwenye dakika 30 za nyongeza, huku VAR ikiweka rekodi ya kugomea mabao manne katika mchezo huo, likiwa na straika Romelu Lukaku, ambalo liliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki wakilalamikia uchoraji wa mistari inayoonyesha mtu aliyeoa kuwa iliyokuwa ya kimchongo na The Blues imenyima bao lale.
Dakika 120 zilikwisha na nyavu za miamba hiyo zilikuwa hazikutishwa kabla ya kushuhudia mikwaju 21 ya penalti ikitinga wavuni, Liverpool wakifunga 11 na Chelsea 10.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Lukaku si bure, kuna mkono wa mtu​

lukaku pic


LONDON, ENGLAND. GUMZO la sasa huko Stamford Bridge ni jina la straika Romelu Lukaku.
Kocha Thomas Tuchel hana namna zaidi ya kumuweka tu benchi mshambuliaji huyo hata kwenye mechi muhimu za Chelsea ikiwamo fainali ya Kombe la Ligi iliyopigwa juzi Jumapili na The Blues kuchapwa na Liverpool kwa penalti 11-10. Shida ilianzia kwa Lukaku kugusa mpira mara saba tu kwa dakika 90 katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace.
Kwa jambo hilo, Lukaku aliweka rekodi akiwa mchezaji aliyegusa mpira mara chache kwa dakika 90 tangu takwimu zilipoanza kukusanywa na Opta msimu wa 2003/04.
Kocha Tuchel alisema: “Hiki si kitu tunachokitaka wala Romelu anachokitaka, lakini pia sio muda wa kumcheka na kumkejeli.”
Katika mchezo wa juzi wa fainali ya Kombe la Ligi, Lukaku aliingizwa dakika 74 kuchukua nafasi ya Mason Mount, lakini kuanzia benchi kwenye mechi hiyo ni kitu kinachozua mjadala mkubwa hasa kwa mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa pesa nyingi, Pauni 97.5 milioni dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka jana akitokea Inter Milan.
Lakini, unaambiwa hivi, Crystal Palace ndio kiboko ya kuwafanya washambuliaji waguse mipira mara chache baada ya kumfanyia hivyo Jamie Vardy wa Leicester City mara mbili tofauti ambapo Aprili 28, 2018, Crystal Palace ilimbana Vardy na kumfanya aguse mpira mara tisa tu kwa dakika 90, huku Oktoba 3, 2021 ilimbana tena na kumfanya aguse mara 10 tu, kabla ya kumfanyia hivyo Lukaku, Februari 19, 2022 ilipomfanya aguse mpira mara saba tu. Balaa hilo.
Hata hivyo, ishu ya Lukaku kugusa mpira mara saba kwenye mechi ya dakika 90 ni mwendelezo tu wa maisha magumu ya mshambuliaji huyo huko Stamford Bridge.
Wiki kadhaa nyuma supastaa huyo wa Kibelgiji alilazimika kuomba radhi kwa mashabiki wa Chelsea baada ya mahojiano na televisheni moja huko Italia, kwamba alidaiwa kukosoa mbinu za Tuchel huku akidaiwa kuwa na mpango wa kurudi Inter. Hata hivyo, Lukaku alisema ametafsiriwa vibaya.
Wachambuzi wa masuala ya soka wanadai kwamba kinachomtokea Lukaku kwa sasa huko Chelsea ni mwendelezo tu wa bahati mbaya zinazowakumbuka washambuliaji wanaokwenda kukipiga kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge.
Hii ni awamu ya pili kwa Lukaku kurudi Chelsea, mara yake ya kwanza ilikuwa kwenye msimu wa 2011/12, ambapo alicheza mechi nane, saba akitokea benchi kwenye rekodi za Ligi Kuu England na hakufunga bao lolote katika mechi hizo kabla ya kupelekwa kwa mkopo West Brom, kisha Everton, ambapo baadaye aliuzwa jumla na kuichezea pia Manchester United kwenye Ligi Kuu England, ambapo alifunga mabao 28 katika mechi 66, mechi 11 akitokea benchi.
Kwa kipindi cha miaka ya karibuni, unaambiwa hivi washambuliaji wa Chelsea wamekuwa wakikumbana na wakati mgumu kwelikweli.
Wanasema dungu hasa linaanzia kwenye jezi Namba 9. Mastaa kibao waliowahi kuvaa jezi yenye namba hiyo hawakutoboa Stamford Bridge, kuanzia kwa Chris Sutton, aliyefunga bao moja kwenye mechi 39, Mateja Kezman mabao saba katika mechi 41, Khalid Boulahrouz mabao sifuri katika mechi 20, Steve Sidwell bao moja kwenye mechi 25, Franco Di Santo mabao sifuri katika mechi 16, Gonzalo Higuain mabao matano katika mechi 18, Alvaro Morata mabao 16 katika mechi 48, Radamel Falcao bao moja kwenye mechi 12 na Fernando Torres mabao 45 kwenye mechi 172. Tammy Abraham naye yalimkuta alipokuwa na jezi hiyo na sasa anafanya mambo yake huko AS Roma. Cheki hapa kile walichofanya washambuliaji wenye majina makubwa huko Chelsea kwenye mechi zao za Ligi Kuu England.

Romelu Lukaku (2021-22) - mabao 5, mechi 17
Lukaku si mchezaji mgeni Ligi Kuu England. Rekodi zake zinasoma amecheza mechi 269, amefunga mabao 118 na kuasisti mara 35. Lakini, kwa msimu huu amecheza mechi 17 na kufunga mabao matano. Katika mechi hizo, Chelsea imeshinda mara 10 na kupoteza tatu akiwa ndani ya uwanja. Mabao yake mawili amefunga kwa mguu wa kulia, mawili kichwa na moja mguu wa kushoto. Mambo yake si mazuri akipambana kumshawishi kocha Tuchel ampe nafasi mbele ya Kai Havertz.

Andriy Shevchenko (2006-09) - mabao 9, mechi 48
Supastaa wa Ukraine, Andriy Shevchenko wakati anakipiga AC Milan alikuwa moto wa kuotea mbali. Huduma yake ndani ya uwanjani ilikuwa balaa zito kiasi cha kumshawishi bilionea wa Russia, mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kuamua kufungua pochi ili kunasa saini yake akakipige huko Stamford Bridge. Baada ya kuvaa uzi wa The Blues tu, kama kawaida majanga ya washambuliaji kwenye kikosi cha Chelsea yaliendelea, ambapo aliishia kufunga mabao tisa katika mechi 48 alizotumikia timu hiyo kwenye ligi. Mambo hayakwenda.

Fernando Torres (2011-15) - mabao 20, mechi 110
Bilionea Roman Abramovich baada ya kumwona Fernando Torres akifanya mambo yake huko Anfield alipokuwa na kikosi cha Liverpool aliona si mbaya akimvuta akakipige kwenye timu yake huko Stamford Bridge. Kwenye hilo, alifungua pochi na kunasa saini ya Mhispaniola huyo kwa ada ya Pauni 50 milioni kwenye dirisha la Januari. Lakini, baada ya kutua Chelsea, Torres ni kama vile alisahau buti zake za kufungia mabao alizisahau huko Anfield, ambapo aliishia kufunga mabao 20 kwenye mechi 110 alizocheza kwenye ligi akiwa na uzi wa The Blues.

Radamel Falcao (2015-16) - bao 1, mechi 10
Kuna ambaye hamfahamu Radamel Falcao? Kama hajawahi kucheza dhidi yake, kumwona mubashara au kwenye luninga, basi atakuwa amemsikia. Straika huyo wa Colombia alikuwa moto kwelikweli ndani ya uwanjani. Huduma yake huko Atletico Madrid iliwafanya AS Monaco kulipa pesa nyingi sana kunasa saini yake. Lakini, mambo hayakuwa mambo alipotua kwa mkopo huko Stamford Bridge, ambapo alicheza mechi 10 za Ligi Kuu England na kufunga bao moja tu. Straika wa aina ya Falcao kufunga bao moja mechi 10 si kitu cha mzaha.

Alvaro Morata (2017-20) - mabao 16, mechi 47
Straika Alvaro Morata alitamba Real Madrid. Juventus wakampenda wakamsajili. Mambo yake matamu huko Serie A, yaliwafanya Real Madrid kumrudisha tena kwenye kikosi chao kwa sababu waliweka kipengele cha kumnunua tena mshambuliaji huyo wakati wanamuuza kwenda Juventus. Baada ya Antonio Conte kutua Chelsea, alihitaji huduma ya Morata na hapo akaenda kunasa kwa ada karibu Pauni 60 milioni. Alipotua Stamford Bridge kila kitu kilitibuka, alifunga mabao 16 katika mechi 47 kwenye ligi na matokeo yake akatolewa kwa mkopo.

Gonzalo Higuain (2019) - mabao 5, mechi 14
Samaki hafundishwi kuogelea ndicho ambacho ungeweza kusema kuhusu Muargentina Gonzalo Higuain kwenye suala la kusukumbia mipira nyavuni. Staa huyo wa zamani wa Real Madrid goli analifahamu vizuri kwelikweli na ndiyo maana baada ya kupiga kazi ya maana huko Napoli, Juventus walipendezwa na kwenda kumsajili kwa pesa ndefu. Baadaye mambo hayakuwa mazuri akijikuta akitolewa kwa mkopo na kuibukia Chelsea, ambapo alifunga mabao matano katika mechi 14 alizocheza kwa ligi. Ulikuwa usajili wa Maurizio Sarri huko Stamford Bridge.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

ABRAMOVICH AIWEKA SOKONI CHELSEA DOLA BILIONI 3​

AVvXsEiJfm7KjfZZ92nzOFdq_hGCwfwKy_E-lWYx27dah5ZZnhXDocFBn8KJdZFZgOEnbGM-Ty7ejSEK06rmUIdrtoxLpTZjX6R91RRTucAi2G4mdgvd8iBZqxEkwoQhf42bugdbcIlqFzCKAZ92Yu3FXOWOaPvkjbQG0QpH55fccyWYbvLtHWFnbn4Mkaiw=w640-h520

VYOMBO vya habari Uingereza vimeripoti kwamba bilionea Mrusi, Roman Abramovich mmiliki wa Chelsea anaiuza klabu hiyo.
Bilionea wa Kiswiss, Hansjorg Wyss yupo kwenye nafasi nzuri ya kuinunua dhidi ya mabilionea wa Marekani kwa dau la dola za Kimarekani Bilioni 3.
Roman Abramovich anatafuta mnunuzi wa haraka wa klabu hiyo baada ya kuwekewa vikwazo vingi kufuatia majeshi yanchi yake, Urusi kuvamia na kuishambulia Ukraine kwa wiki ya pili sasa.
Taarifa zaidi zinasema Bilione huyo aliyeanza kuimiliki mwaka 2003 anauza pia na majengo na mali zake nyingine Uingereza kuepuka kutaifishwa.
Abramovich ameweza zaidi ya dola Bilioni 2 tangu ainunue Chelsea na kuifanya kuwa moja ya klabu kubwa Ulaya na yenye mafanikio zaidi England ikitwaa mataji 19 chini yake na ndio mabingwa wa sasa wa Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Chelsea Yapigwa Kitanzi​

newslite1646977615824.jpg

Mzozo wa kivita baina ya Urusi na Ukraine umechukua mkondo mwingine ambao una madhara ya kusikitisha kwa timu ya kandanda ya Chelsea ambayo mmiliki wake ni bilionea kutokea nchini Urusi Roman Abrahamovic anayetajwa na Uingereza kuwa mmoja wa wawezeshaji wakuu wa sera za rais Vladmir Putin.

Mataifa mbalimbali barani Ulaya yanazidi kuiwekea Urusi vikwanzo vikali vya kidiplomasia na kibiashara kwa kile wanachokitaja kwamba ni taifa hilo kukiuka tahadhari za kiusalama na kuivamia Ukraine.

Uingereza pia imemuwekea mmiliki huyo wa Chelsea vikwazo vingi ambavyo moja kwa moja vinaiathiri timu ya Chelsea na shughuli nyingi timuni humo zinatarajiwa kusambaratika huku wadhamini mbalimbali wakijiondoa na wengine kusitisha mikataba yao na timu hiyo ambayo ndio mabingwa wa dunia kwa sasa.

Baadhi ya vikwazo ambavyo serikali ya Uingereza imemuwekea Abrahamovic na ambavyo vina athari hasi kwa timu ya Chelsea ni kuhusu hisa za timu hiyo, uhamisho wa wachezaji ambapo hakutakuwa tena kutia mikataba mipya na wachezaji katika timu hiyo, tiketi za mechi hazitauzwa wala kununuliwa, timu haitaweza kununua wachezaji wapya na pia mmiliki huyo hatoweza kuiuza timu hiyo isipokuwa aishawishi Uingereza kuwa yeye na Urusi hawatofaidi kitu chochote kutoka kwa uuzwaji wa timu hiyo.

Kipengee kingine katika marufuku hiyo kinasema kwamba Abrahamovic ataweza tu kuiza timu hiyo kama ataikubalia Uingereza kuingilia kati na kuwa mmoja wa washikadau wa kuipiga mnada timu ya Chelsea.

Kufikia Alhamis, tayari kampuni ya Uingereza ya Three ilitangaza kukatisha mkataba wa ushirikiano baina ya timu hiyo na kutaka nembo yao kuondolewa kwenye jezi za timu hiyo huku ikisemekana walikuwa wamekaribia makubaliano ya kuongeza mkataba wa miaka miwili na timu hiyo kabla ya mzozo nchini Ukraine.

Mapema wiki iliyopita mmiliki huyo alikuwa amefikia uamuzi wa kuiuza timu hiyo kutokana na marufuku yake aliyokabidhiwa dhidi ya kuingia Uingereza kwa kile mamlaka yqa taifa hilo ilimtaka kuwa mmoja wa wawezeshaji wakubwa wa sera hasi za rais wa Urusi Vladmir Putin.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

CHELSEA YAIKANYAGA NEWCASTLE 1-0 DARAJANI​

AVvXsEiYkXplWLJOLDSvAo6foRtS9hodhdN4jwQySOqdwWa03PgOaDovy2ddoXMvsToligdDl8_Zy06Wgif49nT4JA6MHcHetbQt_VvpP5i6Jpaz7znh0GQ5aDdBjWundIVYOdGi8Skk_P_KnnRyX4c99uTYvx-BEIbthooRP3bXsjOQf4OVaVFfawowNJFq=w640-h426

BAO pekee la Kai Havertz dakika ya 89 limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Chelsea inafikisha pointi 59 katika mchezo wa 28, ingawa inabaki na nafasi ya tatu, wakati Newcastle inabaki na pointi zake 31 za mechi 28 nafasi ya 14.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Wachezaji wa Chelsea Chalobah, Ziyech na Lukaku wakiwa nchini Marekani kwenye moja ya mechi za mpira wa kikapu ( Basketball
🏀
)



 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

BRENTFORD YAITANDIKA CHELSEA 4-1 STAMFORD BRIDGE​


TIMU ya Brentford jana ilitoka nyuma na kushinda 4-1 dhidi ya wenyeji, Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Chelsea ilitangulia kwa bao la Antonio Rudiger dakika ya
48, kabla ya Brentford kuzinduka kwa mabao ya Vitaly Janelt dakika ya 50 na 60, Christian Eriksen dakika ya 54 na Yoane Wissa dakika ya 87.
Ushindi huo unaifanya Brentford ifikishe pointi 33 katika mchezo wa 31 na kujivuta nafasi ya 14, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 59 za mechi 29 katika nafasi ya tatu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

CHELSEA YAWATANDIKA SOUTHAMPTON 6-0 ST MARY’S​


TIMU ya Chelsea imezinduka kwa ushindi wa 6-0 dhidi ya wenyeji, Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. Mary's, Southampton, Hampshire.
Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na Marcos Alonso dakika ya nane, Mason Mount dakika ya 16 na 54, Timo Werner dakika ya 21 na 49 na Kai Havertz dakika ya 31.
Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 59 katika mchezo wa 29, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi 13 na Liverpool walio nafasi ya pili, nyuma ya Manchester City wenye pointi moja zaidi yao, wote wakiwa wamecheza mechi 30.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
OFFICIAL: Klabu ya Chelsea imethibitisha kuwa mshambuliaji wao Romelu Lukaku atakosa mechi ya Marudiano ya Uefa Champions League dhidi ya Real Madrid kutokana na majeraha yanayomkabili
278190173_5257020164357891_169155743159024604_n.jpg
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA WOLVES​



WENYEJI, Chelsea wamelazimishwa sare ya 2-2 na Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumamosi Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Mabao ya Chelsea yamefungwa na
Romelu Lukaku kwa penalti dakika ya 56 na 58 akimalizia pasi ya Christian Pulisic, wakati ya Wolves yamefungwa na Trincão dakika ya 79 na Conor Coady dakika ya 90 na ushei.
Kwa sare hiyo, Chelsea inafikisha pointi 67 mechi ya 35, ingawa inabaki nafasi ya tatu, wakati Wolves imefikisha pointi 50 katika mechi ya 35 pia nafasi ya nane.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

CHELSEA YAICHAPA LEEDS UNITED 3-0 ELLAND ROAD​


TIMU ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Elland Road, Leeds, West Yorkshire.
Mabao ya Chelsea yamefungwa na Mason Mount dakika ya nne, Christian Pulisic dakika ya 55 na Romelu Lukaku dakika ya 83 na sasa wanafikisha pointi 70 katika mchezo wa 36, ingawa wanabaki nafasi ya tatu wakiizidi pointi nne. Arsenal ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Leeds United ambayo ilimpoteza mchezaji wake, Dan James aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 24 tu kwa kumchezea rafu Mateo Kovacic, inabaki na pointi zake 34 za mechi 36 nafasi ya 18.