Fahamu kuhusu Bitcoin.

Muwekezaji

Mgeni
Dec 10, 2021
10
3
5
Dar Es Salaam
Bitcoin ni fedha ya kidigitali ambayo huondoa uhitaji wa waamuzi na wasimamizi wa fedha kama benki na serikali na badala yake kutumia mtandao wa kompyuta zenye uwezo wa kuthibisha manunuzi moja kwa moja kati ya watumiaji.

Kwa kawaida fedha husimamiwa na Benki kuu pamoja na serikali lakini tukija kwenye swala la Bitcoin yenyewe husimamiwa na watu tofauti tofauti walio katika mtandao wa komputa zinazotumia cryptograpy ambayo ni aina ya ulinzi wa taarifa zinazoweza kusomwa na mtumaji pamoja na mpokeaji tu.

Fedha hii ya kidigitali hutumia teknolojia ya Blockchain katika kufanya miamala.

bitcoin Blockchain ni nini?

Blockchain ni nini?

Blockchain ni kitabu cha kumbukumbu ya miamala kinachotunza taarifa za muamala uliopita, muda wa muamala kufanyika pamoja na taarifa za muamala unaofanyika wakati huo na huzitunza taarifa hizo kwa mfumo wa vitalu ambapo kila kitalu kinawakilisha muamala mmoja. Miamala inavyozidi kuwa mingi hutengeneza mlolongo mrefu wa vitalu.

Kila unapofanya muamala wa Bitcoin unaongeza kitalu cha taarifa katika kumbukumbu ambayo husomwa na kudhibitishwa na komputa zilizo sehemu mbalimbali duniani na baada ya kuhakiki taarifa hizo za muamala huzirekodi na kuzitunza, ifahamike kuwa baada ya taarifa hizi kurekodiwa haitawezekana tena kufanya mabadiliko yeyote.

Pia taarifa zote za miamala huwa wazi katika mtandao wa kompyuta zinazotumika katika kufanya miamala hiyo lakini wanauwezo wa kuona tu taarifa za muamala na sio taarifa za mtumaji wala mpokeaji.

Teknolojia ya Blockchain imeundwa na mambo yafuatayo:

Mtandao – Kuwezesha mawasiliano baina ya watumiaji

Cryptography – Ulinzi wa mawasiliano katika mazingira hatarishi yanayo muwezesha mhusika kuhakiki ujumbe na kuthibitisha uhalali wa ujumbe wake hata kukiwa na wadukuzi katika mtandao.

Consesus Algorithm – Hizi ni kanuni mbalimbali zinazotumika kuongeza kitalu kipya cha taarifa katika kitabu cha kumbukumbu. Ili kompyuta yako iweze kupata nafasi ya kujaza kumbukumbu mpya ni lazima ipate jibu la tatizo la kihesabu linalotolewa ambalo linahitaji uwezo mkubwa wa kumpyuta ili kutatuliwa. Kompyuta yako inapofanikiwa kupata jibu la hesabu hiyo na kulionyesha mtandaoni unakuwa umetoa ushahidi kuwa wewe ndo wa kwanza kupata jibu hilo na hivyo utapokea tokeni au sarafu ya kidigitali ya Bitcoin kama zawadi.