Feitoto kuzikutanisha Yanga na Azam leo usiku
Mechi tatu za ligi kuu ya Kandanda Tanzania bara zinachezwa leo katika viwanja tofauti.
Moja ya mechi yenye mvuto na ushindani ni kati ya mabingwa watetezi Yanga dhidi ya Azam FC.
Yanga na Azam, ukiachia ushindani wao wa uwanjani, pia wapo katika vita juu ya sakata la kiungo Faisal Salum ( Feitoto) ambapo pande zote zinavutana juu ya usajili wake.
Azam inadaiwa kumsajili mchezaji huyo ambaye pia Yanga inadai kuendelea kuwa na mkataba naye.
Tayari mchezaji ameripotiwa kuripoti katika kambi ya Yanga.
Mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa mbili usiku.
Katika mchezo uliopita, timu hizo zilitoka sare ya 2-2 baada ya Feitoto kuisawazishia Yanga mara mbili na kunusuru alama moja.
Ratiba ya mechi nyingine za leo ni kama ifuatavyo:
16:00 || Mbeya City vs Tanzania Prisons
18:15 || Kagera Sugar vs Geita Gold FC