FT : Yanga SC 0 Azam FC 1 | Umeuonaje Mchezo Wa DABI Ya Dar Es Salaam? Una Kipi Cha Kuzungumza Mwana Kijiweni?

MR. VIP

Mgeni
May 17, 2024
25
3
5
Dabi ya Dar Es Salaam imemalizika kwa Matajiri Wa Chamazi kuondoka na ushindi wa bao 1 Kwa 0 dhidi ya Yanga goli likifungwa na Gibril Sillah

Umeuonaje Mchezo Wa DABI Ya Dar Es Salaam? Una Kipi Cha Kuzungumza Mwana Kijiweni?
Mpira ndio ulivyo na matokeo ya mpira huwa katili sana kila mara.
Ukiona umefurahi wewe ujue kuna mwingine kwa matokeo yaliokufurahisha yeye kaumia.

Turudi kwenye mpira kidogo.. timu zetu ni siasa sana kuliko uhalisia.. ukisikia sifa za yanga unaweza sema hata ije timu gani inafungwa tu na haitakuja kutokea yanga kufungwa🤔🤔🤔

Simba na yanga ni maneno tu na wengi wanafungwa nazo kwa maneno tu lkn ni timu za kawaida tu.

Washabiki na viongozi wanasiasa tu wanapenda kusifiwa na hawataki kukosolewa ikitokea timu yao imefungwa basi wanapata pa kutupia lawama.

Kama sio kocha ni refa kama sio refa ni viongozi kama sio wao basi wachezaji wanahujumu 🤣🤣🤣

Tukubali leo azam wamekuwa na nidhamu sana ya mchezo na hawakuwa na papala kabisa roteshen ya wachezaji wa yanga haikuwa tishio leo azizi K leo hajaonekana, Prince Dube kama hayupo, max kajitahidi lkn kapotezwa tu.. yaani naweza eleza woote na jibu likawa moja.

Hongera AZAM FC hongereni Yanga kwa kuwapatia point 3 wapinzani wenu huu ndio mpira tukubali matokeo.
 

Eddy de Jr

Mgeni
May 9, 2024
91
16
5
Utopolo wameisha rasmi. Ukiangalia kwa jicho la tatu,,, Aziz Ki, Chama,Aucho, Dube, Musonda, Mwamnyeto,,, wafyekwe tu dirisha dogo,,, otherwise, mtamaliza nafasi ya kumi.
Afu Kibwana Shomari, Faridi Musa, Denis Nkane, watafute timu zingine,,,, mnawadumaza kwa kuwakalisha benchi.
 
Last edited: