FULL TIME : GUINEA 1 TANZANIA 2 | Leo Mna Lipi La Kuzungumza WAZALENDO?

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
489
643
125
Mchezo wa pili wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika Umemalizika Kwa Tanzania kuondoka na Ushindi wa bao 2 Kwa 1 Ugenini

Mna Lipi La Kuzungumza WAZALENDO Wa Kijiweni?

Wafungaji Wa Magoli

Feisal Salum Abdallah
Mudathir Yahya Abbas
 

MIKOGO 2024

Mpiga Chabo
Sep 10, 2024
4
0
0
Daah aisee Leo ni siku ya Shangwee sana Kwa Sisi Watanzania,, Sina bud kutoa shukran kubwa Kwa Viungo wetu machachari: Fey na Mdathir 💯💯,, Guinea ndo kama anatupa ka nafasi hvii😅😅
 

Gk Never

Mpiga Chabo
May 22, 2024
3
1
0
Mchezo wa pili wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika Umemalizika Kwa Tanzania kuondoka na Ushindi wa bao 2 Kwa 1 Ugenini

Mna Lipi La Kuzungumza WAZALENDO Wa Kijiweni?

Wafungaji Wa Magoli

Feisal Salum Abdallah
Mudathir Yahya Abbas
 

roberts

Mpiga Chabo
Sep 10, 2024
1
0
0
Mchezo wa pili wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika Umemalizika Kwa Tanzania kuondoka na Ushindi wa bao 2 Kwa 1 Ugenini

Mna Lipi La Kuzungumza WAZALENDO Wa Kijiweni?

Wafungaji Wa Magoli

Feisal Salum Abdallah
Mudathir Yahya Abbas
Hakika tumepata faraja lakni star inaimarika kila kukicha pia tangu mechi ya mwanzo imekuwa katika ubora wa Khali ya juu
 

Untouchable

Mpiga Chabo
Sep 10, 2024
4
0
0
Kazi nzuri lakini substitution ya kutoa winger na kuingiza beki ni upuuzi kocha alidhumunia nini but all in all big up
 

njovu master

Mgeni
Jul 24, 2024
10
1
5
Goli la kwanza la Tanzania 🇹🇿 tumefungwa kizembe kutoonesha ushilikiano kama alivyoonesha Ibrahim baka kwanza apewe mauwa yake baka kamwaga jasho kwa ajili ya taifa lake wakupewa lawama pale katka lile goli ni nondo mwamnyeto I think akuwa na kokoto mchanga na simenti na ndiomana akuweza kwenda msaidia baka ingalikuwa alikuwa nyuma yake lakini mchezo ni mzuri leo pesa mama atake asitake razima azitoe tu I love you Tanzania 🇹🇿
 

Rhino

Mgeni
May 8, 2024
10
1
5
Yaani mpaka wasemwe ndio wajirekebishe.
1. Kwanza kabisa kazi nzuri kama timu/wapambanaji tuna faida ya point 4
2. Kuna sehem kadhaa za kuzifanyia kazi
a)Benchi la ufundi liwe makini kwenye kupanga watu sahihi kwa nafasi sahihi sio mtu wa kushoto unamweka kulia kiungo kumweka beki na mengineyo ya kiufundi.
b) Kwenye kuchagua Formation. Kocha achague formation yenye faida sio ya uwoga maswala ya 4_5_1 siyaafiki kama tunahitaji ushindi au points.
3. Kwa wachezaji
a) Wachezaji baadhi hawajitumi yaani kama vile hawana cha kupoteza
b) kuchelewa kufanya maamuzi(wazito) wanakaa na mpira mpaka wanapokonywa badala ya kutoa pasi au kushambulia kama FEI TOTO au MUDA kitu kinachoongeza ubora wao Kila siku.
* c) Hapa inabidi tukubali na tuwe na wivu wa maendeleo na tujifunze kwa wenzetu waliofanikiwa, Wachezaji wetu hawana ubora kama timu Wana Ubora kwa mchezaji mmojammoja kitu ambacho kimewanyima hamasa SAMATTA. Tofauti na timu za wenzetu kama Jana GUINEA walikuwa na ubora wa timu jinsi wanavyoshambulia na kukaba Kila mchezaji alikuwa na ubora. Mfano Sisi tuna FEI, MUDA, MZIZE, ZIMBWE, BAKKA kitu ambacho hatuwezi kujiamini 100% kupata ushindi. Inabidi tuwe na Wachezaji watakaounda UBORA wa Timu kuweza kushindana kimataifa sio kushiriki.
4. Kuwa na Wachezaji wenye uwezo mkubwa hasa wa kimataifa. Najua Kuna changamoto kwa Wachezaji wetu kwenda kucheza ligi kubwa uwezo wanao tatizo ni connection na mawakala wa uhakika wasio wababaishaji wasio na tamaa. Kama hatupati nafasi nje basis tuwape Wachezaji wetu nafasi kwenye ligi ya ndani Ile waweze Kuwa bora.
5. Kuandaa Wachezaji kwa muda wote wapatikane wakihitajika. Tunakuwa na Wachezaji wa muda mfupi wakistaafu tunapata shida ya kuwaanda wengine, tuwe nao muda wote isiwe Kila siku tuna saa wapya.
6. TFF waendeleze miundombinu ya kukuza Wachezaji/vipaji.
MWISHO tusikate tamaa penye Nia Pana njia jitihada zinaonekana tujitume HONGERENI KWA USHINDI WA JANA👏👍
 

willibrod

Mpiga Chabo
Sep 13, 2024
2
0
0
Mchezo wa pili wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika Umemalizika Kwa Tanzania kuondoka na Ushindi wa bao 2 Kwa 1 Ugenini

Mna Lipi La Kuzungumza WAZALENDO Wa Kijiweni?

Wafungaji Wa Magoli

Feisal Salum Abdallah
Mudathir Yahya Abbas
kiukweli matumain yapo .nijambo lakushukuri