Kwa timu yetu ya Taifa stars mimi naona tunakosa vitu vingi sana ambavyo vinapelekea tushindwe kufanya vizuri hasahasa maeneo mawili, eneo la kiungo na ushambuliaji. Ubora kwa wachezaji wetu ni tatizo kubwa mno, dribbling skills, passing, creating chances, hata hizo nafasi chache zinazopatikana hazitumiwi ipasavyo.