Hivi MANULA Si Kapona? Mbona Hayupo Na Simba Pre-Season?

Mshua

Mgeni
May 27, 2024
34
24
5

BADO kesho ya golikipa Aishi Manula haieleweki ndani ya Simba Kwa kuwa mpaka Sasa hajaungana na wenzake Pre- Season inayoendelea Misri.

Taarifa zinadai kuwa, ni kama viongozi hawaoni Sababu ya kuendelea naye tena lakini hofu Yao ni Kwamba asije akaenda timu zingine ikiwemo Azam FC ambao wapo mstari wa mbele kutaka kumrejesha.

Hadi Sasa Manula ameshapona majeraha yake na yupo tayari kuitumikia klabu yake ingawa bado Kuna giza.

Mchezaji huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba na Simba wanajifikiria mustakabali wa Kipa huyo, kama aendelee kuwepo au wamuache akapate changamoto nyingine.

Klabu ya Azam FC inaelezwa kwamba imeiandikia barua Uongozi wa Simba kuhitaji huduma ya mlinda mlango wao Aishi Manula.

 

JeffBunKauga

Mpiga Chabo
Jun 5, 2024
5
0
0
Kila zama na Kitabu chake, wakati wake umepita, ni muda wa Manula sasa wa yeye kutoka Simba na kwenda kutafuta changamoto sehem zingine.