Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati imerejea na itaamza kutimua vumbi Julai 6 hadi 22 mwaka huu visiwani Zanzibar.
Timu zitakazoshiriki ni :-
1. Yanga SC - Tanzania Bara,
2. Simba SC - Tanzania Bara,
3. Azam FC - Tanzania Bara,
4. Coastal Union - Tanzania Bara
5. JKU SC - Zanzibar
6. Vital'O - Burundi,
7. APR FC - Rwanda,
8. Al Merreikh - Sudan,
9. Al Hilal - Sudan,
10. Hai El Wadi - Sudan,
11. Gor Mahia - Kenya,
12. SC Villa - Uganda,
13. Bentiu - Sudan Kusini,
Aidha, timu tatu kutoka nje ya nchi wanachama wa CECAFA zilizoalikwa na kuthibitisha kushiriki michuano hiyo ni TP Mazembe (DR Congo), Nyasa Big Bullets (Malawi) na Red Arrows ya Zambia.