Huyu ndo Kambole aliyekwama Yanga?

Feb 7, 2023
61
36
5
Tangu aondoke ndani ya Yanga kwa mkopo kujiunga Zesco United mshambuliaji Lazaro Kambole amekuwa na kiwango bora sana.

Nyota huyo raia wa Zambia ameshafunga magoli manne kwenye mechi tatu alizocheza ndani ya miamba hiyo ya Zambia chini ya Kocha George Lwandamina.

Najiuliza kambole alikuwa majeraha tangu awasili ndani ya Yanga akitokea Kaizer Chiefs, lakini alivyopona alipewa mechi za kutosha kuonyesha kiwango chake?

Unaweza kusema Yanga walimtoa kwa mkopo kwa ajili ya kumpa Match Fitness, kwanini hawakumpa mechi hizo ndani ya Yanga?

Kambole now prove them he can compete for opportunity 20230212_125212.jpg
 
  • Like
Reactions: kamakawa