Jambo Gani Katika Kauli Za Rais Wa Heshima Na Mwekezaji Wa Simba Unatamani Litekelezwe Haraka Zaidi?

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
466
620
125
"Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kutufikisha wote hapa na kwa niaba ya Wanasimba wote naomba kumpongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu kwa uongozi wake bora na mchango wake mkubwa wa kuendeleza michezo nchini."

"Hii ni safari ya pamoja na kwa pamoja tutafanikisha maono makubwa. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita Simba Sports Club imepata mabadiliko makubwa ambayo yanalemga kuimarisha klabu yetu."

"Kujenga upya Simba kumekuwa na gharama kubwa lakini ni hatua muhimu sana. Tumeweza kusajili wachezaji 14 na Mpanzu tumemleta. Hii ni hatua muhimu katika kujenga kikosi imara ambacho kitaweza kushindana katika ngazi ya juu."

"Tumepata kocha mpya, Fadlu Davids pamoja na benchi mpya la ufundi, kuimarisha miundombinu sahihi ni muhimu katika kufanikisha maono yetu. Tunaendelea kubuni mifumo mipya, bodi imara na kwa pamoja tutahakikisha kila hatua inachukuliwa kwa umuhimu sana."- Mohammed Dewji.

"Ili kufanikisha yote haya tunasubiri mchakato wa mabadiliko ya Simba kukamilika. Tuko katika hatua za mwisho. Ujenzi wa miundombinu hii unakuja na gharama kubwa, ni ngumu kuanza huu ujenzi bila mfumo kubadilika."

"Tukishirikiana tunaweza kujenga Simba inayoweza kushindana ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika, malengo haya sio ndoto, bali ni lengo linaloweza kufikiwa. Pamoja tunaijenga Simba ya kesho."

"Huu ni wakati wa kuchukua hatua kwa nguvu zaidi. Tukimaliza mchakato wa mabadiliko Simba itakuwa tayari kusimama imara na kujitegemea. Kwa heshima kubwa naomba tuache fitna, tuache fitna tuwe kitu kimoja. Tusigawanyike."- Mohammed Dewji.
IMG-20241006-WA0017.jpg
 

hustler

Mgeni
Oct 6, 2024
2
2
5
Huu ni wakati wa kuchukua hatua kwa nguvu zaidi. Tukimaliza mchakato wa mabadiliko Simba itakuwa tayari kusimama imara na kujitegemea. Kwa heshima kubwa naomba tuache fitna, tuache fitna tuwe kitu kimoja. Tusigawanyike."- Mohammed Dewji.
 

*Daniel*

Mgeni
Sep 25, 2024
14
9
5
Mimi ni mwananchi nawatakia mafanikio makolo ktk kile wanachokiamini, kwenye mashindano lazima kuwepo na mshindi.
 

amanigilberth12

Mpiga Chabo
Oct 8, 2024
1
0
0
Actually ameongea maneno mazuri kuhusu umoja na kushikamana kuepuka fitina na mizengwe ambayo ndio chanzo cha mgawanyiko....nadhani mchakato wa mabadiliko umechelewa Sana sijui kwanini wakati simba imeanza muda mrefu kuhusu hii transformation ya club shida nini haikamiliki mpk muda huu?!