Jinsi ya Kununua Bitcoin Tanzania na Jinsi ya Kuuza Bitcoin Tanzania

Muwekezaji

Mgeni
Dec 10, 2021
10
3
5
Dar Es Salaam
Ili kuweza kuuza au kununua bitcoin Tanzania, unatakiwa kuchagua soko (bitcoin exchange) utakalotumia. Yafuatayo ni masoko makuu na yanayoaminika ya kununua bitcoin Tanzania.

Paxful
Paxful ni moja ya kampuni maarufu duaniani na inayoaminika kwa kuuza na kununua bitcoin. Ukitumia kampuni hii kununua au kuuza bitcoin Tanzania, unaweza hata kutumia Tigo Pesa, MPesa, benki, kadi za benki, Western Union, etc. ili kulipia bitcoin au kupokea malipo ya bitcoin unayouza.

BitPesa
Kenya ni kiongozi katika tasnia ya bitcoin katika Afrika Mashariki. Ikiwa na makao yake makuu jijini Nairobi, Kenya, BitPesa ni jukwaa la ubadilishanaji wa fedha za dijiti na malipo. Uzuri wa soko la BitPesa ni kuwa unaweza kuuza na kununua bitcoin Tanzania kwa kutumia pesa za rununu (mobile money) kama Tigo Pesa lakini sio M-Pesa.

Remitano
Unaweza pia kuchagua kwenda na kampuni ya Shelisheli inayoitwa Remitano. Inatoa soko la kuaminika la bitcoin ambalo watu hununua na kuuza Bitcoin nchini Tanzania.

LocalBitcoins
Ikiwa unakusudia kununua au kuuza moja kwa moja bitcoin toka kwa muuzaji au mnuzuzi binafsi nchini Tanzania, unaweza kutumia LocalBitcoins.

Pursa
Pursa ni kati ya masoko ya kununua na kuuza bitcoin Tanzania bila matatizo. Kwenya soko la Pursa, unaweza kununua na kuuza kwa kutumia njia mbalimbali za maliko zikiwemo Ezy Pesa, Airtel Money, MasterCard, Halotel Money, Tigo Pesa, Visa, au TTCL. Kwenye soko hili, huhitaji kujiandikisha ili ununue au uuze bitcoin.

Coinmama
Coinmama ilianzishwa mwaka 2013 na hadi sasa imetoa huduma kwa wateja zaidi ya milioni 2 million katika nchi zaidi ya 180 ikiwemo Tanzania. Ukitumia Coimama unaweza kulipa kwa kutumia kadi za benki, benki, n.k.

YellowCard
YellowCard ni moja ya masoko bora kwa watu wasio na uzoefu mkubwa wa masuala ya bitcoin na sarafu za dijitali. Matumizi ya soko hili ni mepesi kujifunza. Njia ya kulipa au kupokea malipo inayopendelewa na soko hili ni malipo kwa kutumia benki.
 
  • Like
Reactions: Jomo