JKT Tanzania imepanga kucheza mechi yake ya Ligi Kuu dhidi ya Simba, Mei 5, 2025 katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga badala ya Uwanja wake wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam.
Uamuzi wa JKT Tanzania kupeleka mechi hiyo katika Uwanja wa Mkwakwani umechukuliwa baada ya kufungwa kwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati wa mwisho kuupa utayari wa kutumika kwa ajili ya mazoezi ya timu zitakazoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika wa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) 2025 mwezi Agosti mwaka huu.
Tayari JKT Tanzania imeshachagua Uwanja wa Mkwakwani baada ya kuambiwa kufanya hivyo na pua timu yao ya wanawake ya JKT Queens huenda ikacheza mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Simba Queens katika Uwanja wa Manungu Complex, Turiani Morogoro.