Mpaka leo Kibu Dennis amekosekana katika kambi ya Simba kwa siku 16. Ikumbukwe kwamba Simba ilifika Misri Julai 8 na inatarajiwa kurejea Dar mwishoni mwa mwezi huu kabla ya Agosti 3 kuwa na tamasha la Simba Day ambalo huambatana na utambulisho wa wachezaji watakaoitumikia msimu ujao.Kuchelewa kwa mchezaji huyo kuingia kambini kunamfanya Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids kuendelea kuwanoa wengine wanaocheza eneo la ushambuliaji ambalo pia Kibu anacheza.Washambuliaji wa Simba kuelekea msimu ujao ni Jean Ahoua, Steve Mukwala, Valentine Mashaka, Freddy Michael na Kibu ambaye atakuwa na kazi ya ziada ya kufanya ili kuhakikisha anapenya kikosi cha kwanza baada ya kutokuwa kambini huku wenzake wakiendelea kujinoa.