Kijiwe cha Mashabiki wa Real Madrid (‎Los Blancos)

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
485
641
125
Hapa wanakutana mashabiki wa Real Madrid mabingwa mara nyingi zaidi wa Ligi ya mabingwa Ulaya
 

Gamondi

Mgeni
May 27, 2024
18
14
5
REAL MADRID imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya KUMI NA TANO (15) kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi miamba ya Ujerumani, Borussia Dortmund kwenye fainali iliyopigwa katika dimba la Wembley, London.

Borussia Dortmund walikuwa bora sana kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuwaadhibu Mabingwa hao wa Uhispania kabla ya mambo kugeuka kichwa chini miguu juu kipindi cha pili pale Real Madrid ilipogeuka mbogo na kupata magoli mawili.

FT: Dortmund 🇩🇪 0-2 🇪🇸 Real Madrid

⚽ Carvajal 73’

⚽ Vini Jr 82’

Dortmund imekubali kipigo cha pili mfululizo kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zote wakipoteza kwenye dimba la Wembley.

Itakumbukwa miaka 11 iliyopita Dortmund ilipoteza fainali dhidi ya Bayern Munich kwenye dimba la Wembley.