Kijiwe cha watoto wa Jangwani

Gamondi

Mgeni
May 27, 2024
18
14
5
Kijiwe hiki kinawakutanisha mashabiki wa klabu ya Yanga wa hapa Kijiweni ambapo humu yatakua yanapostiwa mambo mbalimbali kuhusu Yanga pekee kama vile wachezaji , mechi za klabu na matokeo ya mechi
 

Mshua

Mgeni
May 27, 2024
34
24
5
Mwamba Huyu Hapa Atajwa Kumalizana Na Yanga

BEKI wa kazi ndani ya FC Lupopo Chadrack Boka anatajwa kumalizana na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kuwa ndani ya timu hiyo msimu wa 2024/25.

Beki huyo mwenye miaka 24 raia wa DR Congo Yanga wanatajwa kumalizana naye mapema kwa ajili ya kuimarisha kikosi hicho kinachonolewana Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa ligi wakiwa na pointi zao 80 msimu wa 2023/24 beki wao wa upande wa kushoto chaguo la kwanza alikuwa ni Joyce Lomalisa ambaye anatajwa kwamba anasepa ndani ya kikosi hicho.

Sababu hiyo imewafanya mabosi wa Yanga kuingia chimbo kusaka mashine nyingine ya kazi mapema wamemalizana na beki huyo ambaye atakuja kuchukua mikoba ya Lomalisa.

Ni kandarasi ya miaka miwili inatajwa kwamba amesaini kujiunga na timu hiyo yenye tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
 

Wisdom

Mpiga Chabo
Jun 2, 2024
1
0
0
Hii ndio fainali ya kibabe kabisa kuwahi ku shuhudia hongera sana kwa chama la wana,wana wa nchi,