Kinachoendelea Kuhusu AUGUSTINE OKRAH Ni Funzo Kwa Yanga

Gamondi

Mgeni
May 27, 2024
18
14
5
Anaitwa Augustine Okrah 'Magic' mchezaji ambaye alisajiliwa ndani ya Yanga SC katika dirisha dogo la usajli, Okrah ni mchezaji mzuri sana na uwezo wake ni mkubwa mno awepo uwanjani.
Kinachoendelea kati yake na uongozi kama ambavyo habari zilivyo ndio kitu ambacho nimeshindwa kukielewa, upo wakati unatakiwa kuvumilia jambo na muda mwingine unashauriwa kutumia mambo taratibu.
Kusajiliwa kwake Yanga SC na kurudi tena nchini ilikuwa ni heshima kubwa kwa upande wake kwaiyo hii alipaswa kuitumia kama fursa kwake ili kuendelea kukiimarisha kiwango chake na kuwajibu wale wote ambao walimuhusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu alipokuwa pale SIMBA SC.
Kama walisema wewe ni Mlevi ilikuwa kuubadili huo na kuuleta mguuni kisha kuwalevya sana wapinzani wako lakini kitendo hiki maana yake inaenda kuwasafisha Viongozi wa Simba ambao walifanya maamuzi ya kuachana na mchezaji huyo.
Hakuna afya katika hili juu yake kama mchezaji wala haimuweki katika mazingira mazuri kwani ndio inaenda kumchafulia taswira ya mpira wake. Nia ya Viongozi ilikuwa ni njema kutaka kukilinda kiwango cha mchezaji lakini yeye ameigeuza na kuifanya kuwa mbovu.
Ngoja nione hadi mwisho itakuaje lakini ni nani atakubali kufanya kazi na mfakazi ambaye akikwama kidogo au wakikwamisha mambo yake kidogo tu yeye anavaa mabomu na kuanza kupambana.