Nashindwa kuwaambia jinsi nilivyojikatia tamaa kiasi cha kuwa kichaa.
Ila ninachoweza kuwaambia tu vijana wenzangu tuacheni kubeti kwa malengo kwamba tunapata pesa huko haraka haraka.
Fikiria nimefanya kazi ya kuajiriwa kwa miaka 8, nikafukuzwa kazi nikaenda NSSF nikachukua milion 7.5 niliyokuwa nakatwa alafu yote nimeimaliza kwenye kindege cha aviator ndani ya siku 5 tu.
Nahisi kuna roho flani iliniongoza kwa sababu kwa akili ya kawaida najiona siyo mimi.
Lengo ilikuwa kubetia elfu 50 kama mtaji wa kubetia lakini kilichofata ni kupoteza milion 7.5 zote bila kubaki hata mia ndani ya siku 5 tu.
Hapa nilipo I wish hata nijitoe roho tu maana sijui ni wapi naanzia maisha tena pesa yote nishaipoteza kwenye uraibu wa kamari.
Kila nikiwaza nna miaka 30, sijaoa, sina biashara yoyote niliyoisimamisha kunilinda, sina maisha, kwa kifupi hiyo milion 7.5 nilitegemea ndiyo niingie nayo mtaani inilinde.
Lakini shetani kanikamata na kunikanda kisawa sawa.
Najiona mjinga wa kiwango cha Phd ndiyo maana nimejiita Zero Brainer, sina wa kumlaumu ila tujiepushe sana na uraibu hasa wa kubeti.
Mimi naweza nikafa leo ila sitaki vijana wenzangu yaje yawakute yaliyonikuta mimi sasahivi.
Mimi hali nnayopitia sasa kwa sababu ya kubeti nakosa maneno ya kuwaelezea ila siku nikifa mjua KINDEGE cha AVIATOR kimesababisha kifo changu .
KAMA UNAWEZA KUNISHAURI NISHAURI PIA NASOMA MAONI YENU