KOMBE LA DUNIA 2022. (QATAR)

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Shirikisho la soka duniani FIFA kwa kushirikiana na Adidas wametangaza mpira utakautumika kwenye Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar
🇶🇦


277510373_5225262787533629_1062785012715882841_n.jpg
277560254_5225262784200296_11326760155289360_n.jpg
277557695_5225262777533630_946773265860297552_n.jpg
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

WATANZANIA WANAOTAKA KWENDA QATAR KOMBE LA DUNIA...​




WATANZANIA wanaotaka kwenda kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini Qatar wametakiwa kutuma maombi ya tiketi kupitia tovuti ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).


 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Fifa Yakanusha Madai ya Kutumika Dakika 100 Kwenye Kombe la Dunia 2022​


batch_infantino.jpg

Rais wa FIFA Gian Infantino
BAADA ya hivi karibuni taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya Fifa kuangalia uwezekano wa kuongeza dakika za mchezo wa mpira wa miguu kutoka 90 hadi 100 kabla ya mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia la nchini Qatar, FIFA imeibuka na kukanusha taarifa hizo.

Taarifa kutoka fifa imesema:
“Kufuatia taarifa za uzushi zilizosambaa leo, FIFA inapenda kuliweka sawa swala hili kwamba hakutakuwa na mabadiliko yoyote yale kuhusiana na muda wa kucheza mpira wa miguu uwanjani katika mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia la nchini Qatar 2022, au katika mashindano mengine yeyote yale.”

FIFA-president-Gianni-Infantino.jpg

Rais wa FIFA Gian Infantino akielezea jambo
Taarifa hizo zimeibuka baada ya Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Masuala ya Michezo CIES kutoa takwimu kwamba zaidi ya dakika 30 zinapotea kwenye kila mchezo wa kawaida wa dakika 90 kutokana na kupoteza muda (Time-wasting) na kurusha mipira inayokuwa imetoka (Throw-ins)
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Refa 'wa Simba' aula Kombe la Dunia​

refa-pic-data.jpg

Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limemtetua refa Jean Jacques Ndala Ngambo kwtika orodha ya awali ya waamuzi wa kati kwa ajili ya kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia baadaye mwaka huu.

Refa huyo kutoka Jamhuri ya DR Congo alizua mjadala hivi karibuni baada ya RS Berkane ya Morocco kumlalamikia kuwa aliipendelea Simba katika mechi ya raundi ya nne ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu ambayo walipoteza kwa bao 1-0.

Hata hivyo malalamiko hayo yalitupiliwa mbali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) na siku chache baadaye refa huyo alipangwa kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia baina ya Misri na Senegal.

Orodha hiyo ya awali ya waamuzi nane wa kati kutoka Afrika imehusisha marefa waandamizi ambao wana historia na uzoefu mkubwa wa kuchezesha mechi kubwa na zenye ushindani wa hali ya juu.

Refa aliyezua mshangao katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zilizofanyika Cameroon mwaka huu, Janny Sikazwe kutoka Zambia naye amejumuishwa katika orodha hiyo ambayo haina jina hata moja la refa kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Marefa nane wa kati kutoka Afrika walioteuliwa katika orodha ya awali ya kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia ni Mustapha Ghorbal (Algeria), Redouane Jayed (Morocco), Bakary Gassama (Gambia), Bamlak Tessema (Ethiopia), Victor Gomez (Afrika Kusini), Janny Sikazwe (Zambia), Maguette N' diaye (Senegal) na Jean Jacques Ndala Ngambo (DR Congo)