Kombe la Shirikisho barani Afrika

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Kikosi cha ASEC Mimosas kimetua jijini Dar Es Salaam
🇹🇿
tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao Simba Sc Jumapili hii Februari 13 katika uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni.
273810120_5090309271028982_3356633570245360575_n.jpg
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1, amesimama na ndani
Inaweza kuwa picha ya Watu 7, watu wanasimama na ndani
273714933_5090309281028981_3026396714029264070_n.jpg
273645570_5090309274362315_6576437293377234615_n.jpg
273653726_5090309287695647_3413012210929629863_n.jpg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Ni Zaidi ya Umafia! ASEC Mimosas Ya Ivory Coast Wajipange.​

273175120_151972573854602_4461920906590845852_n1.jpg

NI zaidi ya umafia! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia kile ambacho Benchi la Ufundi la Simba limekifanya katika
maandalizi kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
Katika umafia huo, Simba wamemtumia beki wao wa kati raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa ambaye amevujisha mbinu zote za wapinzani wao hao jambo lililomfanya Kocha Mkuu, Pablo Franco, kuanza kutabasamu akiona tayari wamepata pa kuanzia.
Simba Jumapili hii, watakuwa na kibarua cha mchezo wa kwanza wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Wawa amewahi kuichezea ASEC Mimosas kwa kipindi cha miaka nane tangu 2003 mpaka 2011 ambapo
alijiunga na Al Merreikh ya Sudan, kabla ya kutua Azam alipocheza 2014 hadi 2016, kisha akarudi Al Merrikh.
Baada ya hapo, 2017 akatua Simba alipo hadi sasa.
ASEC-Mimosas-1.jpg

Akizungumza na Spoti Xtra kuhusu wapinzani wao hao, Wawa alisema: “Najisikia furaha kupata nafasi ya
kucheza tena dhidi ya ASEC Mimosas baada ya kupita takribani miaka 12, hii ni timu ambayo ilinipa nafasi ya
kujulikana na kucheza Sudan na sasa Tanzania.
“Utakuwa mchezo mzuri kutokana na ukweli kwamba wachezaji wao wengi wanatokea kwenye vituo vya
kukuzia vipaji.
“Utamaduni wao kwa kiasi kikubwa ni wa kucheza mpira wa kiufundi na kumiliki zaidi mchezo, lakini sio
wazuri sana katika mpira wa nguvu, hivyo kama tutaweza kuwakaba na kuwashambulia kwa nguvu basi ni wazi
lazima tutapata matokeo mazuri dhidi yao.”
ASEC-Mimosas-2.jpg

Naye Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, alisema: “Tunauelekea mchezo mgumu dhidi ya ASEC Mimosas, lakini niwaweke wazi kuwa tumejipanga vizuri kuhakikisha tunashinda.
“Kupitia njia zetu mbalimbali tumefanya tathimini ya ubora na upungufu wao, hivyo tunajua nini cha kufanya.” Katika Kundi D, mbali na ASEC Mimosas, Simba imepangwa na timu za RS Berkane ya Morocco na Union Sportive Gendarmerie
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Simba, ASEC kitapigwa sana.​

ASEC PIC

ASEC Mimosas ya Ivory Coast, tayari imeshatua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuvaana na Simba katika pambano la kwanza la Kundi D, huku Kocha Mkuu wa Wekundu wa Msimbazi, Pablo Franco akiweka jeshi lake vizuri kwa mchezo huo.
Timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza tangu zilipokutana mwaka 2003 katika mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini rekodi baina yao zinaonyesha kuwa pambano hilo soka litapigwa sana Uwanja Benjamin Mkapa.
Katika mechi hizo za mwaka 2003, Simba ilishinda nyumbani kwa bao 1-0 kisha kunyukwa mabao 4-3.lakini vijana wa Pablo wanatakiwa kuwa makini na Asec hasa kwa kipindi cha pili kutokana na mwenendo iliyoonyesha katika michezo mitano iliyopita kwenye ligi yao ya ndani huko Ivory Coast.
Takwimu zinaonyesha ndani ya michezo hiyo, imepachika mabao 10 na kuruhusu nyavu zao kuguswa mara mbili tu, hiyo inatoa picha kuwa wana safu nzuri ya ushambuliaji yenye wastani wa kupachika mabao mawili kwenye kila mchezo.
Vinara hao wa Ligi Kuu Ivory Coast wamekuwa hatari zaidi kipindi cha pili kwani ndani ya mabao 10 waliyofunga kwenye michezo mitano iliyopita asilimia 80 (mabao 8) wamepachika kipindi cha pili.
Hivyo, Pablo na vijana wake, ambao wamekuwa wakiwatumia kwenye safu yao ya ulinzi wakiongozwa na kipa, Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein, Joash Onyango na Hennock Inonga pamoja na Jonas Mkude ambaye anatumika kama kiungo mkabaji wanapaswa kuongeza umakini.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC YAANZA NA GIA KUBWA MAKUNDI AFRIKA, YAICHAPA ASEC 3-1.​

AVvXsEgm3Bq49gL-NhLI-pCcuJ1lCZJXaRaOV2bl8S7dnINgYhMhYTIGhYNK9YaRq3eogRZ3BjoED_rn1sL52e2FLZFI-KD6K2Rk1YzgfNECNfjSOH66PnKM3Z6zC9UvmmQmK5Ugqtt63T9fKm0YuKtILQjpwt5mk-MXh1HPEq3_NCBVFMt9m6VEmW_SqUJm=w640-h420

WENYEJI, Simba Sports Club wameanza vyema mechi za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya mabingwa wa zamani Afrika, ASEC Mimosas jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 12 kwa til-tak akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomari Salum Kapombe ambaye alifunga bao la pili kwa penalti dakika ya 79.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya kipa wa ASEC, Abdoul Karim Cissé kugongana na winga wa Simba, Yussuf Valentine Mhilu kwenye boksi.
Na ilikuja baada ya kiungo Stephane Aziz Ki kuisawazishia ASEC dakika ya 60, kufuatia kumhadaa beki Mkongo wa Simba, Hennock Inonga Baka ‘Varane’ kabla ya kumchambua kipa namba moja Tanzania, Aishi Salum Manula.
Kiungo wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda akaihakikishia Simba SC pointi tatu katika mechi ya kwanza ya Kundi D kwa bao lake zuri dakika ya 81 akimalizia pasi ya Nahodha, John Raphael Bocco.
Mechi ijayo Simba itakuwa ugenini kuwafuata Union Sportive Gendarmerie Nationale Jumapili ijayo Uwanja wa Jénérali Seyni Kountché Jijini Niamey nchini Niger.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Kocha Berkane Apata Mchecheto, Kucheza na Simba​

Florent-Ibenge-1.jpg

BAADA ya kuzitazama rekodi zake anapocheza naSimba, Kocha Mkuu wa RS Berkane, Florent Ibenge, amekiri
kukutana na upinzani mkali dhidi ya timu hiyo katika michuano ya kimataifa.
Ibenge amekutana na Simba mara nne katika michuano ya kimataifa wakati alipokuwa akiinoa AS Vita ya DR Congo
ambapo katika michezo hiyo amepoteza mitatu na akishinda mmoja.
Ibenge kwa sasa akiwa kocha mkuu wa RS Berkane ya nchini Morocco, anatarajiwa kukutana na Simba katika
mchezo wa Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Februari 27, nchini humo, ambapo timu hiyo imetoka kupoteza katika mchezo uliopita kwa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ibenge alisema kuwa, rekodi zake dhidi ya Simba hazina matokeo mazuri
lakini sio sababu ya wao kushindwa kupata matokeo kwa kuwa wanayo kila sababu ya kupambana na kutafuta matokeo mazuri mara baada ya kupoteza katika mchezo uliopita wakiwa ugenini nchini Ivory Coast.
“Ni kweli rekodi yangu dhidi yao si nzuri lakini sio sababu ya sisi kufeli dhidi yao, kuna nafasi nzuri ya kupambana dhidi yao, tumetoka kupoteza katika mchezo uliopita tukiwa ugenini nchini Ivory Coast, hivyo tunatakiwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani.
“Kwa jinsi ambavyo ilivyo ni lazima tupate matokeo mazuri nyumbani kwa kuwa ugenini sio salama, kila timu imepanga kupata matokeo mazuri nyumbani, Simba wamepata matokeo tayari nyumbani na ugenini na hiyo ni faida kwao, ndio maana utaona kuwa wanaongoza kundi,” alisema kocha huyo.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Tuisila aipiga mkwara Simba​

Tuisila pic

YULE winga wa zamani wa Yanga kwenye kasi ya kishada, Tuisila Kisinda ambaye sasa anaitumikia RS Berkane, ameipiga mkwara Simba akidai hasira ya kipigo walichopewa na Asec Mimosas zitaishia kwao wakati timu hizo zitakapokutana katika mechi itakayopigwa Jumapili hii.
Simba na Berkane zipo Kundi D la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Jumapili usiku zitavaana, kila mmoja ikiwa na kiu ya ushindi baada ya Wamorocco hao kulazwa 3-1 ugenini na Asec, huku Simba ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya USGN.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Morocco, Kisinda alisema matokeo yaliyopita yalikuwa ni bahati mbaya kwao na sasa wanarudi nyumbani kujipanga ili kushinda dhidi ya Simba na kujiweka pazuri kwenye msimamo wa kundi hilo.
“Simba nawajua ni wazuri na matokeo waliyoyapata ugenini yamewapa nguvu, lakini nasi tumejipanga na tunataka tu ushindi dhidi yao bila kuangalia idadi ya mabao,” alisema Kisinda ambaye kasi yake iliwasumbua sana mabeki wakiwamo wa Simba katika Kariakoo Derby.
Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez na Kocha Pablo Franco walisema jana wakiwa Morocco kwamba wameenda nchini humo ili kupata ushindi kwani malengo yao kufika mbali anga za kimataifa.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA YAPIGWA 2-0 NA BERKANE MOROCCO, ASEC HOI NIGER​

AVvXsEgcIgyQqC8HlAkN14j1mbhmxH-RFK7K-mFSvZKH1EiRbjXelhdVLQWg-NjfnPnUmUDrkDSdNYTJbFh970mTJedfkSED3hPefeVWGPIYd54sOO9_xTEtmEVeAACjsxxqGDBten2C49lROqgVZh6D3RG9bodvhYD75dY1aT9b5omxUdfTRNyIju2brA5q=w640-h408

MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamepoteza mechi ya kwanza Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa 2-0 na wenyeji, RSB Berkane usiku wa Jumapili Uwanja wa Manispaa ya Berkane nchini Morocco.
Mabao ya Berkane yote yalipatikana kipindi cha kwanza la kwanza shuti la mpira wa adhabu la kiungo wa kimataifa wa Mauritania, Adama Ba dakika ya 32 na la pili kiungo Mmorocco, Charki El Bahri dakika ya 41.
Mechi nyingine ya kundi hilo jana, wenyeji, Union Sportive Gendarmerie Nationale (USGN) wameichapa AS des Employés de Commerce (ASEC) Mimosas 2-0 mabao ya Wilfried Gbeuli dakika ya 63 na Victorien Adebayor dakika ya 90 Uwanja wa Jénérali Seyni Kountché mjini Niamey nchini Niger.
Sasa Berkane inaongoza Kundi D kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na USGN na Simba zenye pointi nne kila moja, wakati ASEC yenye pointi tatu inashika mkia.
Mechi zijazo ASEC Mimosas watakuwa wenyeji wa USGN Jijini Abidjan nchini Ivory Coast na Simba watawakaribisha Berkane Jijini Dar es Salaam Machi 13.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Kama vipi tukutane kwa Mkapa, Berkane yatibua mambo​

FULL SIMBA PIC

SIMBA ilipoteza mechi ya kwanza kwenye mechi za makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kunyukwa na RS Berkane kwa mabao 2-0, lakini ikajifariji kwa kusema itamaliza kazi Kwa Mkapa.
Simba ilikumbana na kipigo kwenye Uwanja wa Berkane, Morocco katika mechi ya Kundi D iliyopigwa kuanzia saa 4:00 usiku na kuifanya ing’oke kileleni hadi nafasi ya pili ikisaliwa na pointi 4 sawa na ilizonazo USGN ya Niger iliyoitoa nishai ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa kuilaza 2-0 katika mechi ingine ya kundi hilo.
Mabao mawili ya Adama Ba dakika ya 32 na Charki El Bahri dakika ya 41 yakitokana na makosa ya safu ya ulinzi ya Simba ilitibua rekodi ya Mnyama kundini.
Kocha Pablo Franco aliwaanzisha Nahodha John Bocco na Kennedy Juma badala ya Meddie Kagere na Yusuph Mhilu walioanza katika kikosi kilichovaana na USGN na kutoka nao sare ya 1-1 wiki iliyopita.
Berkane ilianza kwa kasi, japo kipindi cha pili Simba ilirudi kivingine baada ya mabadiliko ya kumuingiza Bernard Morrison badala ya Peter Banda na kuungana na Ousmane Sakho kuivuruga Berkane.
Simba sasa itakuwa na nafasi ya kulipa kisasi itakapoialika Berkane Machi 11 kwenye Uwanja wa Mkapa.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Kisinda Aionya Simba Kwa Mkapa​

KISINDA.jpg

WINGA wa RS Berkane ya Morocco, Tuisila Kisinda amesema kuwa kucheza na Simba wakiwa ugenini katika Uwanja wa Mkapa, Dar sio sababu ya wao kupoteza mchezo huo.
Timu hizo zitakutana tena Machi 13, katika uwanja huo baada ya hivi karibuni kuvaana nchini Morocco na Simba kupokea kichapo cha mabao 2-0 ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi.
Kisinda ambaye aliichezea Yanga msimu uliopita ameliambia Championi Jumamosi, kuwa kucheza uwanjani hapo hakuwafanyi wao kupoteza mechi hiyo kwani malengo yao ni kupata matokeo mazuri katika michezo yao yote inayofuata ili wafike mbali.
“Malengo yetu safari hii ni kuweza kufika mbali katika michuano hii, hivyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunafanya vizuri katika kila mchezo uliosalia ili tuweze kutimiza malengo yetu.
“Sisi kucheza katika Uwanja wa Mkapa siamini basi itakuwa asilimia zote kwamba Simba watashinda mchezo huo, tunahitaji kupata matokeo mazuri tukiwa kwao japo wamekuwa na historia nzuri wakiwa katika uwanja wao,” alisema winga huyo.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Ibenge Aihofia Simba Kwa Mkapa​

Florent_Ibenge.jpg

KOCHA wa RS Berkane ya Morocco, Florent Ibengé amesema kuwa mpira wa Simba wanapokuwa katika uwanja wao wa nyumbani ni kikwazo kuelekea katika mchezo wao wa marudiano wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba wanatarajiwa kuwakaribisha RS Berkae katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kufanyika Machi 13, katika Uwanja wa Mkapa. Simba wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 2-0 ugenini.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Ibenge aliweka wazi kuwa anazikumbuka mechi ambazo amekutana na Simba katika Uwanja Mkapa huku akiwa na kumbukumbu ya kutokupata hata sare jambo ambalo linampa wakati mgumu kuelekea katika mchezo huo.
“Hakuna ambacho hakipo wazi, nimepoteza michezo mingi, sina kumbukumbu ya kushinda dhidi ya Simba katika uwanja wao, ni rekodi mbaya kwangu lakini sitaki kuona ikijirudia safari hii kwa kuwa kuna mengi yamebadilika katika mpira sio historia mara zote.
“Malengo yetu ni kushinda michezo mingi zaidi ili tuweze kusonga mbele katika michuano hii, katika kundi letu utofauti unatakiwa kuuonyesha katika kupata matokeo ya ugenini, tunatakiwa kufanya hivyo,” alisema kocha huyo.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Morrison amchimba Mkwara Ibenge “Kwa Mkapa Hutoki”​

74063710.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Simba Sc, Bernard Morrison ‘BM3’ amemkaribisha Kocha wake wa zamani, Florent Ibenge nchini Tanzania huku akimtisha kuwa katika mchezo wao na Simba, hawatatoka salama katika Dimba la Mkapa.
Ibenge ambaye ni Kocha Mkuu wa RS Berkane ya Morocco aewasili Tanzania na timu yajke hiyo jana Alhamisi, Machi 10, 2022 kwa ajili ya mchezo wa raundi ya nne hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaopigwa Jumapili Machi 13.
Kupitia Ukurasa wake wa Isntagram, Morrison ameandika; “Whenever I see you, it reminds me of the day you brought me from Ghana to Congo DR and told me that you will help me grow The rest is history the only sad thing is that at Mkapa Stadium we forget what you’ve done nobody survives here.

Welcome to Dar Es Salaam Father
Kila nikikuona inanikumbusha siku ambayo ulinitoa kutoka Ghana hadi Congo DR na kuniambia utanisaidia kukua Mengine ni historia cha kusikitisha tu ni pale kwa Mkapa Stadium tunasahau ulichofanya. Hakuna anayepona hapa.
Karibu Dar Es Salaam Baba.”


Katika mchezo wa kwanza kati ya Simba na Berkane uliopigwa Morocco, Simba aliambulia kichapo cha bao 2-0, hivyo ana kila sababu ya kuhakikisha anautumia vizuri uwanja wa nyumbani kuhakikisha anapata alama tatu muhimu.
Ikumbukwe kuwa, Morrison aliwahi kuitumikia AS Vita Club ya Congo DR msimu wa mwaka 2016, ambayo Kocha wake mkuu alikuwa Ibenge.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Berkane: Simba Itafika Fainali CAF​

simba-7.jpg

KOCHA Mkuu wa RS Berkane ya nchini Morocco, Florent Ibenge, amesifu ubora wa kikosi cha Simba kinachoundwa na nyota kibao, akiwemo Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal, huku akiitabiria timu hiyo kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mchezo wa nne wa Kombe la Shirikisho Afrika kunako Kundi D, kumalizika kwa Simba kuwafunga Berkane bao 1-0, likifungwa na Sakho, juzi Jumapili.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ibenge alisema Simba wameonekana kujiandaa vizuri na michuano hii ambayo malengo yao ni kucheza fainali, hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chao msimu huu.
Ibenge alisema katika michuano hii Simba wameonekana kucheza kwa malengo ambayo yamewawezesha kupata matokeo mazuri katika michezo migumu ikiwemo sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya US Gendamerie ya nchini Niger.
“Kitendo cha Simba kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa miaka minne kumewajenga vema, ninaamini katika Shirikisho watafanya vizuri msimu huu.
“Niwatabirie Simba kucheza fainali ya Shirikisho msimu huu kutokana na uzoefu wao walioupata wa ushiriki wa michuano hii mikubwa Afrika kwa miaka minne mfululizo.
“Simba wamejiandaa vizuri, ni wazi inaonesha wana kikosi imara na chenye malengo makubwa, hivyo nilitarajia upinzani tofauti kabla ya kukutana nao katika mchezo huu,” alisema Ibenge.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MANULA AOKOA PENALTI MBILI, SIMBA YAPIGWA 3-0​

9CDCB84A-3849-458F-A42E-F30B2F4A185D.jpeg

MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamechapwa mabao 3-0 na wenyeji wahamiaji, ASEC Mimosas katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Jénérali Mathieu Kerekoumjini Cotonou nchini Benin.
Mabao ya ASEC yamefungwa na viungo Aubin Kramo Kouamé dakika ya 16, Mburkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 25 na mshambuliaji Karim Konaté dakika 57.
Lakini sifa zimuendee kipa namba moja wa Tanzania, Aishi Salum Manula kwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti ya Konaté dakika ya 36 na mshambuliaji mwingine, Anicet Alain Oura dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo, ASEC inafikisha pointi tisa na kupanda kileleni kwa Kundi D, ikizizidi pointi mbili Simba na RSB Berkane ya Morocco, wakati US Gendamarie inaendelea kushika mkia sasa ikifikisha pointi tano baada ya wote kucheza mechi tano kuelekea mechi za mwisho wikiendi ijayo.
Wakati ASEC watamalizia ugenini dhidi ya Berkane, Simba watamalizia nyumbani na US Gendamarie kuwania nafasi mbili za juu ili kwenda Robo Fainali.
Simba ndio inaongoza Kundi D kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na RSB Berkane pointi sita sawa na ASEC, wakati USGN inashika mkia kwa pointi zake tano.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BERKANE WATOZWA FAINI MILIONI 250 FUJO DHIDI YA SIMBA​

simba%20v%20berkane%20@binzubery.jpg

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeitoza faini klabu ya RS Berkane ya Morocco faini ya jumla ya dola za Kimarekani 108,000, zaidi ya Sh. 250 za Tanzania kwa kufanya vurugu kwenye mechi zote mbili za nyumbani na ugenini dhidi ya Simba.
Katika mechi hizo za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika, nchini Morocco mashabiki wa Berkane waliwatupia vitu wachezaji wa Simba Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Februari 27, mwaka huu wenyeji wakishinda 2-0 na kwa kosa hilo wametozwa faini ya dola 8,000.
Na kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, wenyeji Simba wakiibuka na ushindi wa 1-0 Machi 13, Makamu wa Rais wa Berkane, Majjid Madrane alivamia uwanjani na kuwaongoza wachezaji wake kuwafanyia fujo marefa.
Kwa kosa hilo, Kamati ya Nidhamu ya CAF kwanza imemfungia Madrane kujihusisha na shughuli zozote za soka zinazotambauliwa na bodi hiyo ya kandanda barani kwa mwaka mmoja pamoja na kumpiga faini ya dola za Kimarekani 100,000.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
USGN TAYARI WAPO MJINI
Kikosi cha US Gendermerie ya Niger
🇳🇪
kikiendelea na mazoezi katika Uwanja wa Gwambina Lounge jijini Dar Es Salaam kuelekea kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Simba SC utakaopigwa Jumapili hii katika uwanja wa Mkapa
🇹🇿

Inaweza kuwa picha ya Watu 12, watu wanasimama, nyasi na maandishi yanayosema 'USON USGN USGN USGN'
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Adebayor Awaandalia Sapraizi Simba Uwanja wa Mkapa​

Victorien-Adebayor-87-scaled-1.jpg

KIUNGO mshambuliaji wa US Gendarmerie, Victorien Adebayor, ameweka wazi kuwa atahakikisha anapambana kwa nguvu ili kuisaidia timu yake kupata ushindi dhidi ya Simba,Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho utapigwa Jumapili ya Aprili 3, unatarajia kuwa mkali kwani kila timu ina nafasi ya kwenda robo fainali ikiwa itashinda mchezo huo, wageni wanatarajia kutua nchini kesho Alhamisi.
Licha ya hivyo, Adebayor ambaye amefunga mabao matatu kwenye michuano hiyo anahusishwa kutakiwa na Simba na hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Try Again aliweka wazi kuwa wangependa kumsajili nyota huyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Adebayor alisema kuwa. “Licha ya mchezo huu na Simba kuwa muhimu sana kwetu na kwao ila nitakuwa na furaha sana kuwaona mashabiki wa Simba na kuweza kucheza nao nyumbani.
“Kwa upande wangu maandalizi ya mchezo huo yapo vizuri na sina presha yoyote kuelekea mchezo huo na nitajitahidi kufanya vizuri ili kuisaidia timu yangu.”