SIMBA NA GENDAMARIE KUCHEZWA SAA 4:00 USIKU
MCHEZO baina ya wenyeji, Simba SC na US Gendamarie ya Niger utachezwa muda mmoja na mchezo mwingine wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, RSB Berkane na ASEC Mimosas Jumapili.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeamua mechi zote zianze Saa 4:00 usiku ili kuondoa uwezekano wa upangwaji matokeo iwapo michezo hiyo itachezwa muda tofauti.
Wakati Simba watakuwa wenyeji wa US Gendamarie Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ASEC watakuwa wageni wa Berkane Uwanja wa Manispaa ya Berkane nchini Morocco, Saa 4:00 usiku.
ASEC ndio inaongoza Kundi D kwa pointi zake tisa, ikifuatiwa na Berkane na Simba zenye pointi saba kila moja, wakati Gendamarie ina pointi tano, maana yake timu zote zinaweza kumaliza nafasi mbili za juu na kwenda Robo Fainali.