KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM SPORTS.

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

SIMBA NA DAR CITY JANUARI 28, YANGA NA MBAO TAREHE 29.
AVvXsEiA-SckWhli52AEHupE8HcL7BT_6GSgv63cxxZoTlAm0-wQv-Ju30IpPLDHqiTeoafmkhLJrGjAAHO--daQem-jp_D3uFkhQJ85Xch59_KhqudX0GpaJ_tsen9GHpswMLSda4wFcdOHKTHAjkUz8TTl2JEwCxWeqFbaGt4TglmmX2wabq6coI0jjvb3=w640-h426

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetaja tarehe za michezo wa Hatua ya 32 Bora ya Kombe la shirikisho hilo, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Katika ratiba hiyo, Azam FC watakuwa wenyeji wa Transt Camp Januari 28 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, wakati Yanga watamenyana na Mbao FC Januari 29 na mabingwa watetezi, Simba watacheza na Dar City Januari 30, mechi zote hizo mbili zikipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MECHI YA YANGA NA MBAO ASFC SASA MWANZA.​

AVvXsEjzzQYNQ6XWNSdku1sDudN4i7LaHQNTHfLdk6ZOo7H-wWgPSTrxoI9iGO2YQPRDsWjcZ9-9a1w9BossVql9vGPk5P-OdPwIVs9NTgrAlwyGN84BKTSrwbu5938v6gcEnYFYfBohJy-MFXjuUEni5yYCUfd-Rt5-dlGGx55Y20W-0D9Ad2DQ62ASUlQW=w640-h626


MCHEZO wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baina ya Yanga SC na Mbao FC uliopangwa kufanyika Dar es Salaam Jumamosi sasa utafanyika Mwanza siku hiyo hiyo.

AVvXsEgoFGjYJtvBqvOqb8SBV_Lv6K-RhQgr3QS0MeLTqqXxTlozZ2NE-Tr2gSUboYC_ZEGnkX4wW5ZLlvL0aHNWb9U6C3pH4OzMtaJq5PABfEvLq5Z_zR2WQcCgsxizcoq4foiXetwI74hKAPTMY_Q3Ed79rfJORgcu2W87C4NBs1HcA6dA0P5Ei0C2tuwK=w518-h640
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

DODOMA JIJI, POLISI ZASONGA MBELE KOMBE LA TFF.​

AVvXsEgWmvfJ0gdlhep7ad_TAHuzzbFcZwdnrcK4BNfixM5pJVzQmMxm32FwQkLCqWdDLB1s93bHq6VSZ8z6kiKyJN-Zva-EhoBzFnP2FdG4W4SziRCIbskJkHFgDyzJG4YriWLcmiPNtq6G8b5FB5ippPng7TnQXeaqd-HXYp4H2emnRmuuq-Z6xa06NB0v=w640-h536


TIMU ya Dodoma Jiji FC imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Sumbawanga United usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na Khamis Mcha mawili, moja kwa penalti dakika ya tisa na lingine dakika ya 22, wakati mengine yamefungwa na Seif Abdallah Karihe dakika ya 30 na Anuary Jabir dakika ya 80.
Mechi nyingine za 32 Bora michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Polisi Tanzania imeitoa Ndanda FC kwa kuichapa 3-1, wakati Bagamoyo Friends imeitoa Catamine kwa kuichapa 2-1.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

YANGA WAKIIFANYIA MAZOEZI MBAO FC LEO KIRUMBA.​

AVvXsEg0FWLtBtHdyQqrkPL5X_VNUTeU3pKBWQnDiEe2Bx_0jpmnyPmA2ls1B8JUXiws8j25QE2QZ_T1-FxNnPAh8JwftUexIisNm3SztUwz8aL35fF-S8Ht4W-2fA3XQJunsn3gBs8rTuvtlvjzZ69naEQ_tg2I09g-UYuMgGVv7lsXx0zWixAF-PUC70na=w614-h640


KIUNGO mpya Mkongo wa Yanga, Chico Ushindi akifanya mazeozi leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kujiandaa na mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Mbao FC.
AVvXsEiKw9osbJvPSZEF7-BhmwvNQKbek5_HH382wZgd4s1u_xaui98Iut_5acoZvRDK6t7k6md8EP3FPNgbmM9_R1aQKpDLvZL-fmTOkQSFsXDEVqlebfcWHCOEmgIHx3wxYFR2j2QXu8aMLcqMPlbtqYV4DepVr0Vl0StKKeV8UfPp2PG_T4k_YmR2OffP=w614-h640

Kiungo mpya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ akifanya mazeozi leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbao FC Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
AVvXsEiiMSmbWeE8-W9eMIt_5W0p61wq-TIY_8j4x7sPZkIZqb0Y9DQB1k9uqLVm8h8brPi6LkJlwV78_MfypYmzL6vSnmLeDSmhCDiRC98yXyCRiS3C9SmpxcmoICMV1Uz2bCXLBhUgRMG-1DO93-Mw0SOx2iZ09jalRpuLyYSD3mG9hXQVTkKbWyUZy3mc=w616-h640


Wachezaji wa Yanga wakifanya mazeozi leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbao FC Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC WAREJEA KUPOZA MACHUNGU KWA DAR CITY.​

AVvXsEghheWcpRlssZlA6c44b_3h2pweEpJzLBDRrQVGBEz7c6_zkamhla3iQHp1N2Ceki_hpu7lPVKOpf3CnbPsj4cdwEuWuIAv3M8-CpZ-icWLhMH99Z-opwobxkxgsn77eslxcqzpRa0b8_I-Ntj-pvBUU7W8bz0pii4h2HW_1pjbsTASYaPcxI1v23aY=w640-h428

MSHAMBULIAJI Mkongo wa Simba SC, Chris Kope Mutshimba Mugalu aliteremka kwenye ndege baada ya ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kutoka Bukoba ambako jana walifungwa 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba.
Simba SC itateremka tena dimbani Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salam kumenyana na Dar City katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Ikumbukwe Simba haijapata ushindi katika mechi tatu zilizopita kufuatia kufungwa 1-0 mara mbili, nyingine na Mbeya City na sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar, zote ugenini.
AVvXsEjXOYjxjBsLf55zrJqEv35RBwHGTSKDDqkWYVy4wcllsLITvTJwKLL59o0m8WCoBFBYmpIdlB4PJ-7y9l1hHxZqMVaCdmtvqdrDs5oIXWnQuRYwOwwDA4AaDEWuK-VlTSCyDtYHcdGOxq7Ey-_JVmBcINwxqcPyv_lHOvQu0bFeMOMkiD6KpFrRM0Hf=w640-h428

AVvXsEhuR7NXvgXEWoCE5riO55jwE1sfrxifcDxQdxEZPEG_glZIeKiV_TacdB5UcIPjtKbRvcb6bPlmBl_9A4QXuTcAZFx1zuJypDUPW88eSdMM3f9KIUqKC0_R0fdAtm2rsJNPg1IDA5-f7_x9Vxyy1EOYhuE2mQ5y0mRzW8CmJ5LrbwqivjQ5UaDOyUpd=w640-h428

AVvXsEhU3nfz9eclRtYW2Ql9jl1RRZxk4n-quwrKNHuupoUfM7m-fdyT-vsZN63CCl8kX0Id3iGpAJmsJ3ME3JPJFUU8bBhDGS6gTuhR1im5hYOjircAyGFkEwE9Dh3FWrcT4IM2K6VvM9UclE9np-A7VgrmpxynxAjK6kXzSE0ea_fKJTAmXHoRwtZaAuHr=w640-h428
AVvXsEgb7reL6CI1LyocQuXbOoJJE5UcUZyW1ijmeZw_Slcm35wx2UhcXje0OK4ViA-ilBjAnSjvcuQxNdwrJWJc0iEO7ovlbtMI_R5I8YwRU5ifIZ7UoGr_UOn3EaBPsdXkEe0-X7TUVbdei7a1qutBgKOgZwGc4smkg0biCBxRDpNZgcv-K-ijDRtb9qQq=w640-h426
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

AZAM, NAMUNGO NA PAMBA ZASONGA MBELE ASFC .​


BAO la Nahodha, beki mkongwe Aggrey Morris dakika ya 30 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Transit Camp katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Azam FC inakwenda Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ambako itamenyana na timu ya Daraja la Kwanza, Bagamoyo Friends iliyoitoa Catamine jana.
Mechi nyingine za leo za Azam Sports Federation Cup, Namungo FC imeitoa Lindi United kwa kuichapa 2-0 Uwanja wa Ilulu mjini Lindi na Pamba FC imeitoa Stand United kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mabao yote ya Namungo yalifungwa kwa penalti na Shiza Kichuya na Ibrahim Mkoko, wakati ya Pamba yalifungwa na Willy Magai na Moses Msukanywele .
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

MAYELE AIPELEKA YANGA 16 BORA KOMBE LA TFF.​


VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza jioni ya leo.
Bao pekee la Yanga leo limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Mkongo Fiston Kalala Mayele dakika ya 54 kwa kichwa akimalizia krosi maridadi ya kiungo mzawa, Farid Mussa Malik kutoka kulia.
Matokeo ya mechi nyingine ya 32 Bora ASFC , Ruvu Shooting imeitoa KMC kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji l Dar es Salaam.
KMC ilianza vizuri kwa kutangulia na bao la Iddi Kipagwile, kabla ya Abrahaman Mussa kuisawazishia Ruvu Shooting na kwenye mikwaju ya penalti kipa Benedict Tinocco alipngua shuti la Kenny Ally.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC YAFUTA GUNDU KWA DAR CITY, YAICHAPA 6-0.​

AVvXsEhP8OWpjFIl2N5ATJAAQVg-0mTOEvzkFWqJaUGJIAXW3s0ldLBp8QCgRstT_GIlWhlrXWGV3tcsWmHwXXk_ovpilZyI6h1LEMqbU7tgxRPfOYsOKGrDpUDwjJT0n3p7LWplgkcdCzJKdbM-CV4kEDsfgxjgy0iPP-p4saPgfifx-8fKwDQycOKOvgjh=w640-h426

MABINGWA watetezi, Simba SC wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Dar City usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na wageni watupu, mshambuliaji Mnyarwanda mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere mawili dakika ya tano na 13, viungo Wazambia, Clatous Chama dakika ya 18 na Rally Bwalya dakika ya 22, beki Muivory Coast, Pascal Wawa dakika ya 48 na mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu dakika ya 80.
Mechi nyingine za 32 Bora leo, Mtibwa Sugar imewatoa wenyeji, African Sports kwa penalti 4-2 baada y sare ya 0-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na Kagera Sugar imewachapa wenyeji, African Lyon 4-0, Meshack Abraham akipiga hat trick, lingine akifunga Abeid Athumani.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

NANI KUCHEZA NA NANI 16 BORA ASFC.​

AVvXsEhxJeF14iORYK13CK13-8EJOYISOY7Fs1TVU3nFTkbsAfxeFu1huUfAWNqAxiwMKOR7NE3xf0yglmwj0MD4kCNahyoBbOhjVdt7LtBG0CDBeyOrbfdQEXPdpRgI2LixhtdFkicFEOUaG_bR1g55Lg2e32f61QTGOwmZxhTQrQePV4QM5Fpe6wbZeFnp=w640-h640

MECHI za Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) zitachezwa mwishoni mwa Februari zikihusisha timu 13 za Ligi Kuu, moja ya Championship ambayo ni Pamba na mbili za Daraja la Kwanza, ambazo ni Baga Friends na Mbuni FC.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Pancha ya gari yamtibulia Hitimana.​

pancha pic

KOCHA Mkuu wa KMC, Thierry Hitimana amesema kuwa sababu kubwa ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ni uchovu kwa wachezaji wake.

Kauli hiyo kwa Hitimana inakuja baada ya kuondoshwa kwenye hatua ya 32-Bora dhidi ya Ruvu Shooting kwa mikwaju ya penalti 6-5 katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

“Gari yetu ilipata pancha wakati tunaenda uwanjani na ilitubidi kukaa kwa zaidi ya saa mawili kusubiri matengenezo, hali ambayo ilisababisha wachezaji wangu kupata uchovu na kukosa fitness,” alisema Hitimana na kuongeza;

“Tuliona kama mchezo tuliumaliza kipindi cha kwanza hasa baada ya kuwa tunaongoza na wapinzani wetu walibadilika kipindi cha pili na kusawazisha bao lililowapa hali ya kujiamini na kututoa mchezoni.”

Naye Mshambuliaji wa kikosi hicho, Matheo Anthony alisema: “Bingwa anapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Shirikisho Afrika hivyo utaona ni kwa jinsi gani ina umuhimu, mpira unapofikia katika hatua ya penalti kinachoamua huwa ni suala la bahati tu.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MECHI ZA 16 BORA ASFC KUCHEZWA KATIKATI YA MWEZI ZOTE.​

RATIBA ya Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetoka na mechi zote za michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) zitachezwa katikati ya mwezi huu.
Azam FC na Baga Friends watacheza Februari 12 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Yanga SC na Biashara United Februari 15 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na mabingwa watetezi, Simba SC watakuwa wageni wa Ruvu Shooting Februari 16 Uwanja wa Mkapa pia.

AVvXsEiStiObLCpcqgvYPa2sgFxOqK_bxtuATQ_Wlb7WVsCRFPM07JOUGAEgDTmiq50yajUjJnhFJssMBt0ukYe3JVONkeFFdYhTHTCQ-6Lkj0LlTSlNyYQru-r9D_Jw6Hnw5QtCFwALwDC-oPwaosfNNzinnFxDQWG95uYZSNqHD4gp6m4PZbBj3m1B0uzq=w640-h640
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

AZAM FC YAPASHA KUIVAA BAGA FRIENDS JUMAMOSI.​


KIUNGO wa Azam FC akifanya mazoezi kujiandaa na mchezo wake wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Baga Friends Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
MECHI ZA 16 BORA ASFC
FEB 12

Baga Friends v Azam FC
Mbuni FC v Geita Gold FC
FEB 14
Coastal Union v Mtibwa Sugar
Kagera Sugar v Namungo FC
FEB 15
TZ Prisons v Polisi TZ
Yanga Sc v Biashara United
FEB 12
Pamba v Dodoma Jiji- Mwanza
Ruvu Shooting v Azam FC
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Biashara United yawaandalia sapraizi Yanga.​

Biashara PIC

TIMU ya Biashara United imeanza rasmi mazoezi katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa Februari 15.
Timu hizo zinakutana kwenye hatua ya 16, bora mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Timu ya Mwanaspoti leo ilikuwa uwanjani kushuhudia timu hiyo inayonolewa na Bahati Vivier wakifanya zaidi mazoezi ya mbinu.
Vivier aliwataka wachezaji wake wacheze mpira wa chini na utulivu huku zoezi hilo likionekana kueleweka.
Wachezaji hao walikuwa wanacheza bila kuwa na goli la kufunga hali ambayo iliwafanya muda wote kuufuata mpira.
Yanga ilifuzu hatua hiyo baada ya kuiondosha Mbao FC kwa bao 1-0 kwenye hatua ya 32, huku Biashara United ikitinga hatua hii kufuatia kuiondosha Mbeya Kwanza mabao 2-1.
Hii ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana msimu huu baada ya awali kukutana kwenye Ligi Kuu Bara Decemba 26, 2021 ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

COASTAL NA KAGERA ZATINGA ROBO FAINALI ASFC.​

AVvXsEjqxxQH8q2kvP06YsD9b149gb9muU5meUbA1gyCI7oJY5GOhEUKTSN7DGABx1JtVTkyyvAF0LxThYw9HtAtPfsWi0STNyhgZJVGMcyQPBzPBUVOslzTqjcQNqTjswOiiKTGKciK8R56iZ2dNptzol_PPbHL0cIMfep8oGx_3UrWhCWszWwWAFFriNGw=w636-h640

TIMU za Coastal Union na Kagera Sugar zimefanikiwa kuingia Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi dhidi ya wageni, Mtibwa Sugar na Namungo jioni ya leo.
Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga mabao ya Coastal Union dhidi ya Mtibwa yamefungwa na Haji Ugando dakika ya 10 na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 90 na ushei na Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera bao pekee la Kagera limefungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 60.
Coastal na Kagera zinaungana na Geita Gold iliyoitoa Mbuni FC na Azam FC ilitoitupa nje Baga Friends kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

YANGA NA POLISI ZATINGA ROBO FAINALI ASFC.​

AVvXsEjB5tKAtqPdrVFnkMkm7T-y4L1c8XeRNIUEniJMUzoLPn8nR4pjv4eqi0SH1zsVULbkblh9AktvilUzRhf_Mra0csmgWqZ6tKPL0XaPjzXEQZldNsiZGHjP2sBHhxJe5ffzwJPG2kyurZRBPJTbyRaBIRoIaRQQrh6pcu_tuoca30ZT8cWLnwoGXL93=w640-h524


VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Biashara United usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC yote leo yamefungwa na nyota wake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), beki Yannick Litombo Bangala dakika ya 22 na mshambuliaji Fiston Kalala Mayele dakika ya 28, wakati la Biashara United limefungwa na mshambuliaji Mkenya, Collins Opare dakika ya 38.
Katika mchezo uliotangulia, Polisi Tanzania ilifanikiwa pia kwenda Robo Fainali ya ASFC baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons mabao ya Said Khamis dakika ya 40 na Daruwesh Saliboko dakika ya 83 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Timu nyingine zilizofuzu Robo Fainali ni Azam FC iliyoichapa Baga Friends 6-0, Geita Gold iliyoichapa Mbuni FC 1-0, Coastal Union iliyoichapa Mtibwa Sugar 2-0 na Kagera Sugar iliyoilaza Namungo FC 1-0.
Hatua ya 16 Bora ya ASFC itakamilishwa kesho kwa michezo mingine miwili, Pamba na Dodoma Jijini Mwanza na Ruvu Shooting dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC Jijini Dar es Salaam.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Bwire: Tunawaondoa Simba FA.​

masau.jpg

RUVU Shooting kuelekea mchezo wao wa leo Jumatano wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (FA) utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar dhidi ya Simba SC, wamesema kuwa wapo tayari kulishangaza taifa.
Akizungumza na Champion Jumatano, Mkuu wa Idara ya Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kuwa, wamefanya maandalizi makubwa kuelekea mchezo huo ili kuhakikisha wanamuondoa bingwa mtetezi wa kombe
hilo, Simba.
“Tumejipanga kuhakikisha tunabadili fikra za watu wengi kwamba timu yoyote itakayo kutana na Simba au Yanga basi haitoweza kupata matokeo, Ruvu ni timu kubwa yenye wachezaji wenye ubora wa hali ya juu hivyo wajiandae kula kipigo kizuri kutoka kwetu.
“Nawaambia Simba waje kucheza mpira, wasithubutu kuja na matokeo yao mfukoni kwa sababu ni kitu ambacho kitakuja kuwaletea madhara makubwa sana baada ya dakika 90 za mchezo.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC YATINGA ROBO FAINALI ASFC KIBABE HASWA.​

AVvXsEj_y3ZxZQlpZ7x_FUfpkaLXejXC5ALhQe7kkoIfmWBWZ2vdcnNYx5XLXiarlT2fVfTUy5S3Kz4aBORq64zuZ3Shtx0_noT5nVqQ53ODPCWizF9jPppBeib0SZOvdfd-MY3xWNakE_CNtech67W9AIE3-tupjxxZmVBBDhtFL-gjsSQwMG8oCkb5C3g7=w640-h416

MABINGWA watetezi, Simba SC wametinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kishindo baada ya ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na Nahodha, John Bocco mawili dakika ya pili n 40, Clatous Chama matatu dakika ya 23, 25 na 73, Masinda aliyejifunga dakika ya 44 na Jimson Mwanuke dakika ya 70.
Timu nyingine zilizofuzu Robo Fainali ni Azam FC iliyoichapa Baga Friends 6-0, Geita Gold iliyoichapa Mbuni FC 1-0, Coastal Union iliyoichapa Mtibwa Sugar 2-0, Kagera Sugar iliyoilaza Namungo FC 1-0, Polisi Tanzania iliyoipiga Tanzania Prisons 2-0, Yanga SC iliyolaza Biashara United 2-1 na timu pekee isiyo ya Ligi Kuu, Pamba ambayo imeitoa Dodoma Jiji FC.
Droo ya Robo Fainali itafuatia wiki ijayo na mechi za hatua hiyo ya Nane Bora zitachezwa mwezi ujao.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

PAMBA YATINGA ROBO FAINALI ASFC.​

AVvXsEjGNnK5mfchkgRSJj0j0fLj7rH4NIT9JVAqZ2MbUyppK6GhkOFhWLqPU0xCNdguizIsoPPfRdabgqaZx9BUsFeCJWzITZuU6LNMzvLpkD6nhmPuBQ6Kpj3h4NmtdKyPHpOYonndkPeNUizxekYy5gNhASjYnwCC92TOgEQRrKQwSHtf2svww6ZpXl3E=w640-h480

WENYEJI, Pamba FC imekuwa timu pekee ya daraja la chini ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Mabao ya Pamba, mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Muungano nchini yamefungwa na Makiada Makoli dakika ya 15 na Masunga Malulu dakika ya 77, wakati la Dodoma Jiji FC limefungwa na Cleophace Mkandala dakika ya 47.
Timu nyingine zilizofuzu Robo Fainali ni Azam FC iliyoichapa Baga Friends 6-0, Geita Gold iliyoichapa Mbuni FC 1-0, Coastal Union iliyoichapa Mtibwa Sugar 2-0, Kagera Sugar iliyoilaza Namungo FC 1-0, Polisi Tanzania iliyoipiga Tanzania Prisons 2-0 na Yanga SC iliyolaza Biashara United 2-1.