KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM SPORTS.

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

ASFC: Simba Kuivaa Pamba, Yanga Dhidi ya Geita​

274489630_377713003711847_7080660980597823825_n.jpg

DROO ya mechi za kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) hatua ya robo fainali imefanyika leo Februari 21, ambapo Yanga watacheza na Geita Gold, Simba watakipiga dhidi ya Pamba, Azam na Polisi na Coastal Union wakipepertana na kagera Sugar.
Kwa mujibu wa droo hiyo mshindi kati ya mechi ya Yanga na Geita Gold, atakutana na mshindi kati ya Simba na Pamba katika hatua ya nusu fainali ya kwanza.
Mshindi kati ya Azam na Polisi atakutana na mshindi kati ya Coastal na Kagera Sugar katika hatua ya nusu fainali ya pili.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Moja tu Simba, Yanga kinapigwa​

robo pic

MASHABIKI wa soka Tanzania huenda wakashuhudia kipute cha watani wa jadi Simba, Yanga kwenye nusu fainali ya kombe la Shirikisho Azam (ASFC) kama kila mmoja itashinda mechi yake ya robo fainali.
Katika upangaji wa droo leo Februari 21 robo fainali ya kwanza itawakutanisha Yanga dhidi ya Geita Gold na mshindi wa mchezo huo ataenda kucheza na mshindi wa robo fainali ya pili kati ya Simba dhidi ya Pamba huku mechi hizo zote zikichezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Yanga wana kazi ya kufanya mbele ya Geita ili kujihakikishia kwenda nusu fainali kutokana na walipokutana kwenye Ligi Kuu Yanga walipata ushindi wa 1-0 huku mchezo ukiwa na ushindani mkubwa.

robo pic 1

Simba na Yanga mara ya mwisho kukutana kwenye mchezo wa nusu fainali ilikuwa Julai 12 huku Simba wakishinda 4-1.
Kulingana na namna ambavyo droo imechezeshwa timu hizo hazitokutana katika fainali kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Msimu uliopita timu hizo zilicheza fainali na Simba walipata ushindi wa 1-0 uliochezwa katika uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Robo fainali ya tatu itawakutanisha Azam dhidi ya Polisi Tanzania na mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa robo fainali ya nne utakaowakutanisha Coastal Union dhidi ya Kagera Sugar.
Hatua ya robo fainali itaanza kuchezwa April 8-13 huku nusu fainali ikitarajia kuchezwa Mei.
Upande wa nusu fainali mchezo wa kwanza utachezwa kwtika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha huku nusu fainali ya pili ukichezwa CCM Kirumba.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mzee Dalali Awataka Yanga SC Nusu Fainali ASFC​

Capture-2.jpg

MWENYEKITI wa Baraza la Wazee la Simba, Hassan Dalali amefunguka kuwa anatamani kikosi chao kikutane na Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) ili wajitengenezea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo.
Simba wana uwezekano mkubwa wa kukutana na Yanga kwenye kombe hilo endapo timu hizo zitashinda mechi zake za robo fainali. Simba wamepangwa na Pamba huku Yanga wakitarajiwa kucheza na Geita Gold.
Mzee Dalali ameliambia Championi Jumamosi, kuwa: “Nina imani tutapata matokeo kwenye mechi ya robo fainali ili tuweze kutinga hatua ya nusu fainali na tunawaombea wenzetu Yanga wapate matokeo dhidi ya Geita ili tukutane nao kwenye hatua ya nusu fainali tuwafunge vizuri.
“Msimu wa 2020 tuliwafunga mabao 4-1 kwenye nusu fainali pia msimu uliopita tuliwafunga kwenye mchezo wa fainali kule Kigoma, hivyo Yanga ni timu ambayo tumeifunga mara nyingi kwenye michuano hii na tunatamani pia tukutane nao kwenye hatua ya nusu fainali ili tuendeleze ubabe dhidi yao.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

YANGA KUKATA UTEPE ROBO FAINALI ASFC​

VIGOGO, Yanga SC ndio watakata utepe katika Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kumenyana na Geita Gold Aprili 10, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
17DE5748-0632-46D2-8265-CA3BFC62E8FB.jpeg
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

COASTAL NAYO YATINGA NUSU FAINALI ASFC KWA MATUTA​



WENYEJI, Coastal Union wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Erick Mwijage alianza kuifungia Kagera Sugar dakika ya sita, kabla ya kiungo Mcameroon, Vincent Abubakar kuisawazishia Coastal Union dakika ya 68.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

YANGA YAENDA KUISUBIRI SIMBA NUSU FAINALI ASFC​


VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa penalti 7-6 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Geita Gold walitangulia kwa bao la Offen Chikola dakika ya 87, kabla ya Yanga kusawazisha kwa bao la mkwaju wa penalti wa beki Mkongo, Djuma Shabani dakika ya 90 na ushei.
Waliofunga penalti za Yanga ni Saido Ntibanzokiza, Yanick Bangala, Fiston Kalala Mayele, Jesus Moloko, Djuma Shabani, Bakari Mwanyeto na Dickson Job, wakati kipa Djigui Diarra alipiga nje.
Upande wa Geita Gold waliofunga ni Yussuf Kagoma, George Mpole, David Kameta ’Duchu’, Adeyoum Ahmed, Offen Chikola na Kelvin Yondan, wakati wachezaji wawili wa zamani wa Yanga, viungo wote walikosa, Maka Edward iligonga mwamba na Juma Mahadhi ilifikia mikononi mwa kipa Diarra.
Sasa Yanga itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya mwisho kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na Pamba FC ya Mwanza.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

AZAM FC YAICHAPA POLISI 3-0 KUTINGA NUSU FAINALI ASFC​


WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Rodgers Kola dakika ya 24, Ismail Aziz Kader dakika ya 45 na Mudathir Yahya dakika ya 78 na sasa Azam FC watamenyana na Coastal Union ya Tanga iliyoitoa Kagera Sugar.
Timu nyingine iliyotinga Nusu Fainali ni Yanga ambayo imeitoa Geita Gold na itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya mwisho baina ya mabingwa watetezi, Simba na Pamba.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA NA YANGA KIINGILIO NAFUU 10,000 KIRUMBA​


KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya watani, Simba na Yanga ni Sh. 10,000 Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Taarifa ya TFF imesema viingilio vingine ni Sh, 30,000 VIP A na Sh, 20,000 VIP B na mchezo utaanza Saa 9:30 Alasiri.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

MAKOCHA, MANAHODHA SIMBA NA YANGA WAELEZA MIPANGO​


KOCHA Mkuu wa kikosi cha Yanga, Nassredine Nabi, amesema kesho hawata waachia simba nafasi ya kutinga fainali kwani msimu huu malengo yao ni ubingwa wa Kombe la Shirukisho la Azam ( ASFC) .
Yanga wanashuka katika dimba la CCM Kirumba saa Tisa Alasiri, kuvaana na mabingwa watetezi wakombe hilo Wekundu wa Msimbazi Simba SC.
Watani wajadi hao kwa msimu huu walikutana mara ya mwisho Mei 30 katika mchezo wa Ligi Kuu nakushindwa kuonuonyeshana umwamba kwakumaliza mchezo huo kwa suluhu kwenye Uwanja wa Mkapa.
Akizungumza na Bin Zubery leo katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Gold Crest Mkoani Mwanza, Kocha Nabi alisema kesho hawata bweteka katika kulipambania nafasi ya kutinga fainali ya ASFC.
Alisema mchezo huo nitofauti kabisa namchezo wa ligi hivyo wataingia kwa tahadhari na malengo yao yakiwa nikuwafunga wapinzani wao.
"Tutaingia Kwa tahadhari maana mchezo huu nitofauti nawaligi kwahiyo nia namalengo yetu nikupata ushindi mechi hii ndio funguo ya kwenda fainali lazima tupambane, " alisema
Kwa upande wake kocha wa simba Pablo Martin, alisema Yanga wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo lakini yeye amejipanga na baadhi yawachezaji wake ambao walikuwa maheruhi wamerudi nawatajiunga nakikosi kesho.
Alisema hawezi kuwataja wachezaji hao kwani atakuwa anataja silaha kwa maadui lakini mchezo utakuwa mgumu nawatajitahidi kupambana kutimiza malengo yao waliyojiwekea.
" mchezo nimgumu na Yanga wanaonekana kama wana nafasi kubwa yakushinda lakini sisi tupo kamili natutajitahidi tuweze kuingia katika fainali kuutetea ubingwa, " alisema.