Kujiondoa Kwa AZAM TV Kwenye Kuonesha Mchezo Wa NGUMI Una Lipi La Kuzungumza Mwana Kijiweni?

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
282
396
25
Watanzania kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiufuatilia sana mchezo wa ngumi baada ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Azam Tv katika miaka ya hivi karibuni baada ya kupotea katika ramani kwa muda mchezo huu lakini LIMEIBUKA jambo ambalo limewashtua wengi na hili ni baada ya maaamuzi ya Azam media kusitisha rasmi kuonesha mchezo huu ni wazi kuwa hili ni pigo kubwa sana kuanzia kwa mabondia wenyewe, walimu wao, mapromota, mashabiki na taifa kwa ujumla. Wewe una lipi la kuzungumza mwana Kijiweni

KUMBUKA KUWA: Mahakama imeamuru Azam Tv kumlipa Mwamakula kiasi cha Shilingi Milioni 200 kutokana na kutumia mashindano ya Vitasa bila ya yeye kunufaika kwa chochote, huku taarifa zikidai kuwa Azam Tv walikata Rufaa ya kesi hiyo na kwasasa Azam Tv ikionyesha kutokuwa na mpango tena wa kuonesha mchezo wa Masumbwi.
 
Last edited:

SNAZY Gasper

Mgeni
Sep 3, 2024
11
5
5
Hii itaasili sana mchezo huo kwani sioni muendelezo mzuri na ufanisi wa kampuni yoyote ya MICHEZO kufanya matangazo ya mchezo huo,cha zaidi inatakiwa Taifa lisimame kidete kuendeleza mchezo huo kwa kufanya maonyesho kwenye channel Kama TBC na zingine za kiserikali
 
  • Like
Reactions: Kijiweni

Rhino

Mgeni
May 8, 2024
10
1
5
Ni sahihi ni pigo kwa watu wote Hao. Nadhani ukiona Kuna changamoto ktk maswala ya investment na advertisement Kuna maswala ya hela. Kwamba Kuna watu wanataka kupata pesa Bila ya kufanya kazi ndio maana company(media) kubwa kama azam TV kujitoa kuepusha uswahili ama ubabaishaji. Angalizo* mamlaka zinazoshughulikia zifwatilie kwa makini... 🖊️ @rhinoking75
 
  • Like
Reactions: Kijiweni

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
282
396
25
Ningependa kujua Azam walitoa sababu zipi za kujitoa
KUMBUKA KUWA: Mahakama imeamuru Azam Tv kumlipa Mwamakula kiasi cha Shilingi Milioni 200 kutokana na kutumia mashindano ya Vitasa bila ya yeye kunufaika kwa chochote, huku taarifa zikidai kuwa Azam Tv walikata Rufaa ya kesi hiyo na kwasasa Azam Tv ikionyesha kutokuwa na mpango tena wa kuonesha mchezo wa Masumbwi.
 
macha

Mgeni
Sep 19, 2024
1
1
5
Kiukweli azam tv imefanya michezo ipendwe na wengi ikiwemo me mmoja wapo ambae mwanzoni nilkua sifatiliagi kabisa ila ilipoanzishwa azam tv ilinipa ushawishi mkubwa sana ikianza kujitoa ivi kuna watu nao wataanza kurudi nyuma kimichezo
 
  • Like
Reactions: Kijiweni

Saidy

Mgeni
Jun 5, 2024
64
16
5
Hakuna jambo lisilo kuwa na sababu. Mpaka wameamua kusitisha mpango wa kuonyesha mchezo huo basi kuna kitu nyuma.. iwe hasara walizopata au kuto kunufaika. Yote kwa yote sisi mashabiki tumeumizwa sana hasa kwa wale tuliokua tukitaza mchezo huo kwa runinga.. ni pigo kubwa lakini kuna mambo wazingatia na hawajataka kuyaweka bayana. Tunawashukuru sana kwa mda ambao tulifurahia nao katika mchezo huo.
 
  • Like
Reactions: Kijiweni
Sep 19, 2024
1
1
5
Itaathiri pakubwa sana, watanzania wengi tulikua hatufuatilii mchezo wa Boxing wa Tanzania Kabisa, tulianza baada ya azam kujihusisha na kuonyesha mchezo huo.

Ofcourse, ni mengi yanaweza kuwa yametokea nyuma ya pazia, lakini kusema ni jambo la faida na hasara, sizani kama linamashiko kivile kwa sasa, sababu, kiuchumi faida haiwezi kupimwa kwa mwaka mmoja au miwili, mpk atleast miaka mitano au zaidi ya investment,

So kwa maoni, wizara husika, ingefuatilia nini kipo nyuma ya pazia, na kama ni kweli ni issue za harasa na faida, basi, tutafute mpango mkakati mzuri, ili wawekezaji wa mchezo huu waweze kupata chochote.
 
  • Like
Reactions: Kijiweni

mbatte

Mgeni
Sep 5, 2024
4
2
5
Me nadhan Tanzania walaji kwa Ganda la ndizi ni weng kuliko wamwaga jasho nadhan Kun kitu kipo kwa wahusika wa ngumi ila acha inyeshe tujue panapovuja Azam TV hawan deni kwetu🏅🙏🙏🙏
 
  • Like
Reactions: Kijiweni

FUNGO JR

Mgeni
May 18, 2024
12
3
5
Nimejaribu kufuatilia kwenye mambo ya kuchukua haki za matangazo nimeona kumekua na ushindan mkubwa sana sasa apa haijulikani kama Azam kashindwa au kaona anaingia hasara lolote linawezekana 🤷
 
  • Like
Reactions: Kijiweni

shulle

Mpiga Chabo
Sep 19, 2024
1
0
0
Hii itapalekea kushuka kwa maendeleo ya mchezo wa ngumi na kupote radha ambayo tulikua tunaipata awali kwa sababu azam TV ndio walikua wanahamasisha na kuutangaza mchezo wa ngumi; kwa uwanda moana sana tofauti na media zingine!!!!
 
Saidi Moses machungi

Mpiga Chabo
Sep 15, 2024
3
0
0
Mimi bi
Watanzania kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiufuatilia sana mchezo wa ngumi baada ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Azam Tv katika miaka ya hivi karibuni baada ya kupotea katika ramani kwa muda mchezo huu lakini LIMEIBUKA jambo ambalo limewashtua wengi na hili ni baada ya maaamuzi ya Azam media kusitisha rasmi kuonesha mchezo huu ni wazi kuwa hili ni pigo kubwa sana kuanzia kwa mabondia wenyewe, walimu wao, mapromota, mashabiki na taifa kwa ujumla. Wewe una lipi la kuzungumza mwana Kijiweni

KUMBUKA KUWA: Mahakama imeamuru Azam Tv kumlipa Mwamakula kiasi cha Shilingi Milioni 200 kutokana na kutumia mashindano ya Vitasa bila ya yeye kunufaika kwa chochote, huku taarifa zikidai kuwa Azam Tv walikata Rufaa ya kesi hiyo na kwasasa Azam Tv ikionyesha kutokuwa na mpango tena wa kuonesha mchezo wa Masumbwi.
Mimi binafsi serikali ingilie kati hili swala,mchezo huu wangumi ulileta ajira kwavija kiasi kwamba mabondia watanzania,waliiperusha bendera ya taifa,Azam tv media waombwe kuendelea kurusha mchezo wa ngumi,ila aingie mkataba namabondia wote Tanzania,kwakipengele maalumu,ili mabondia wafidie deni la bondia mwenzao,ili nawao ajira yao iendelee kurushwa,napia kama serikali anauwezo wakukununu Gori Moja la simba au yanga,basi hili nalo wanauwezo wkuliingilia kati.