Kuna wachambuzi hapa bongo huwa siwaelewi linapokuja suala la mpira, je! Ni mimi tu!

Bakari

Mgeni
May 27, 2024
27
31
5
Hapo nyuma kulikua na mechi za ku Qualify kombe la dunia, na mashindano mengine, na nadhani wengi wenu mliangalia mechi hizo, ila baada ya mechi kuisha sijaona timu kubwa kama Morocco n.k tukiwekewa matokeo, na hii sio mara ya kwanza kwa timu za kiarabu kutowekewa matokeo pale tu wanaposhinda, ila wakifungwa utaona wachambuzi hawa wakiwahi kupost, hivyo sijajua shida ni nini, chuki ama ubaguzi kwa hawa wenzetu!


Mtu anaacha kupost matokeo ya mechi muhimu za ku Qualify kombe la dunia tena ya Morocco aliekiwasha, na akazisumbua timu kubwa kama Portugal na ufaransa w/cup 2022, na kutuwakilisha wa afrika 😄 halafu anakuja kutuwekea matokeo ya friendly matches za akina Portugal, Finland, Iceland, Luxembourg n.k 😃 aisee!


Hivi huwa mnawaelewa wachambuzi hawa? Hata kama utawachukia na kutotuwekea matokeo ya timu zao ilaa wachambuzi wakubwa na waliobobea wanatambua ubora wao hawa jamaa, so, wamebarikiwa kwanzia timu za taifa hadi vilabu wako vizuri,especially Morocco, egypt, Raja na Al Ahly. Mimi ni mmoja wa mafans wa Morocco 🇲🇦


So, Napinga sana ubaguzi, Mungu aniepushie mbali ubaguzi, wivu na chuki.
 
  • Like
Reactions: Amosi Simon

De hexane jr

Mgeni
Jun 10, 2024
4
1
5
Wachambuzi wa bongo ushabiki na unazi ni mwingi katika soka kuliko kazi
Wengi wao hawatumii weredi waliousomea na kuupata huko vyuoni badala yake wanakuwa machawa na kutumiwa na vilabu kuipotosha familia ya mpira.
 

B5emanuel

Mpiga Chabo
Jun 14, 2024
2
0
0
Hakika kuna wachambuzi wazuri lakini waache kuiga kutoka kwa waandishi wengine wa habari maana wengine ni waongo tu