Kuvunja Mkataba wa Jobe Simba Wanatakiwa Kulipa Million 700

Gamondi

Mgeni
May 27, 2024
18
14
5
UNAMKUMBUKA PAR OMAR JOBE? Strika la Magoli aliyeshindwa kufanya maajabu ndani ya Mitaa ya Maimbazi, tangu atue Simba katika dirisha dogo.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amesema kwamba hawafikirii kuachana na mchezaji Par Omar Jobe kwani ni mchezaji mzuri.

Murtaza Mangungu alizungumza hayo kupitia Clouds FM, alipokuwa akifafanua juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea kwa sasa ndani ya klabu hiyo.

“Mkataba wa Jobe ni mrefu kidogo sidhani kama tutaweza kuuvunja, kwanza sio mchezaji mbaya ni mchezaji mzuri na nilimtembelea, tumezungumza na tutaendelea na mchakato wa kuimarisha kiwango chake.” — Murtaza Mangungu.

Mkataba wa Par Omar Jobe ili kuuvunja klabu ya Simba inapaswa kulipa fidia ya Tsh Milioni 700, kwani alisajili kwa miaka miwili na hadi wakati huu ametumikia mkataba wake kwa miezi 6 pekee.

Kuhusu usajili wa Ismael Sawadogo pia ambaye ni mchezaji aliyeshindwa kuonesha kiwango kizuri, na kupelekea kuachwa na Simba Mangungu alisema;

“Yeye amezungumzia wachezani wawili Sawadogo na Jobe , bahati mbaya Sawadogo wakati anakuja pre season aliumia , lakini alikuwa anatoka kwenye timu yao ya Taifa sio mchezaji wa kiwango kidogo”

“Mimi ninachosema hapa atokee mtu anipe timu 5 ambazo wamesajili na wachezaji wote waliosajiliwa wamefanya vizuri,Wallah mimi wala sisubiri kitu ,kesho najiuzulu”

Kinacho endelea katika klabu ya Simba, wanachama ba mashabiki wanashinikiza Mangungu na wajumbe wake wajiuzulu, hivyo kinachotakiwa ni kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa Dharula kama ambavyo katiba ya Simba inasema.
 

Kifundo jr

Mpiga Chabo
May 27, 2024
3
0
0
Kinachoonekana hapa Ngungu na wenzake wanafanya kusud kuchukua wachezaji wenye viwango ambavyo haviendani na klabu ili hapo baadae wamvunjie mkataba wakilipa na wao wapate chochote kitu
 

Bruno Jewel

Mgeni
Jun 4, 2024
5
1
5
Jobe atatakiwa aonyeshe makali yake, mana siamini kama Jobe sio mchezaji mzuri ila upepo mbaya wa timu huwa na tabia ya kufifisha uwezo wa wachezaji
 

Eddy de Jr

Mgeni
May 9, 2024
91
16
5
Mangingu na wenzake ni wahuni,,,unampaje mchezaji kama Jobe mkataba aa miaka miwili???
Mbona mnataka kuifilisi timu makusudi??
Au hiyo ndo vision yenu???