Kuzuiwa na polisi kwa mkutano wa wanachama wa Simba, ni mpango wa Yanga na sio Mangungu

May 27, 2024
7
2
5
Kuna namna wanahitaji kuendelea kutawala soka la Tanzania kwa msimu mwingine na hivyo wanafurahia sintofahamu hii hasa kipindi hiki cha usajili.

Tunawafahamu polisi mashabiki wa yanga lakini pia tunafahamu jinsi wanasiasa walio madarakani wanavyojaribu kuitumia Simba kutimiza ndoto za marafiki zao kisiasa.

Ukweli polisi hawakuwa na sababu ya kuzuia mkutano wa wanachama wa Simba kwani hiyo ndiyo ilikuwa njia ya kujaribu kutatua changamoto zilizopo kuliko kuwaachia viongozi ambao ndio tatizo haswa.

Unakuwa na mwenyekiti mjeuri na mwenye majibu ya kashfa kwa waliompigia kura, unakuwa na wajumbe wa bodi wapuuzi wanasema wanataka kuuweka vizuri mfumo huku kwa miaka mitatu walikuwemo kwenye mfumo wakitumikia bila kufanya chochote huku wakijua kuna tatizo.

Siafiki kabisa kusema eti Mangungo hakuwa na nguvu ya maamuzi kwa hiyo eti anaonewa. Kusema kweli huko ndio kunahalalisha kutokufaa kwake kwa kuwa kama aliona kuna tatizo kwa nini hakuliweka wazi na badala yake alianzisha majungu na wachambuzi fulani fulani ambao kusema kweli huenda ndio wanafaidika sana na migogoro ya Simba.

Ukiona mchezaji kama Jobe amepewa mkataba mrefu ukijiuliza alivyopatikana unaweza kukuta kuna watu wajinga kama akina dauda wanahusika.

Natoa rai kwa hawa viongozi wa polisi wanaotumika, wasiingilie mambo ya kiraia kwa nia ya kuipendelea club wanayoishabikia
 
fat jooh

Mpiga Chabo
May 29, 2024
2
0
0
Naweza kusema BADO simba ipo kwenye rada nzuri kisoka, kikubwa sajili zinazofanyika muda huu na thank you zitakazo tokea ndio zitatupa majibu kuwa tumepotea au msimu ujao ubigwa ni wetu

inshallaah
 
Roy Creation

Mpiga Chabo
Jun 16, 2024
9
0
0
Yanga kuhusika ni uongo coz hata kama polisi ni shabiki wa Yanga from nowhere hawezi kuzuia kitu cha simba bila order maalumu Yanga tuko busy na kitabu chetu cha Historia inakuaje tukawazingue Madunduka
 
Makoye Malonja

Mpiga Chabo
May 15, 2024
8
0
0
32
Geita
Te
Kuna namna wanahitaji kuendelea kutawala soka la Tanzania kwa msimu mwingine na hivyo wanafurahia sintofahamu hii hasa kipindi hiki cha usajili.

Tunawafahamu polisi mashabiki wa yanga lakini pia tunafahamu jinsi wanasiasa walio madarakani wanavyojaribu kuitumia Simba kutimiza ndoto za marafiki zao kisiasa.

Ukweli polisi hawakuwa na sababu ya kuzuia mkutano wa wanachama wa Simba kwani hiyo ndiyo ilikuwa njia ya kujaribu kutatua changamoto zilizopo kuliko kuwaachia viongozi ambao ndio tatizo haswa.

Unakuwa na mwenyekiti mjeuri na mwenye majibu ya kashfa kwa waliompigia kura, unakuwa na wajumbe wa bodi wapuuzi wanasema wanataka kuuweka vizuri mfumo huku kwa miaka mitatu walikuwemo kwenye mfumo wakitumikia bila kufanya chochote huku wakijua kuna tatizo.

Siafiki kabisa kusema eti Mangungo hakuwa na nguvu ya maamuzi kwa hiyo eti anaonewa. Kusema kweli huko ndio kunahalalisha kutokufaa kwake kwa kuwa kama aliona kuna tatizo kwa nini hakuliweka wazi na badala yake alianzisha majungu na wachambuzi fulani fulani ambao kusema kweli huenda ndio wanafaidika sana na migogoro ya Simba.

Ukiona mchezaji kama Jobe amepewa mkataba mrefu ukijiuliza alivyopatikana unaweza kukuta kuna watu wajinga kama akina dauda wanahusika.

Natoa rai kwa hawa viongozi wa polisi wanaotumika, wasiingilie mambo ya kiraia kwa nia ya kuipendelea club wanayoishabikia
Tena huyu anaejiita Shaf sijui saffii Dauda naona kama ana poshen yake Simba sijawahi ona mchambuzi mpuuzi kama huyu cjajua Nia yake niipi🏹