Kwanini SHAFFIH DAUDA Anapinga Kurejea Kwa Mo Dewji Uongozi Simba?

Bakari

Mgeni
May 27, 2024
27
31
5
Dauda amepinga uwepo wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, kwa kusema Simba inatakiwa kuwa ya Mwenyekiti Mangungu.

“Mashabiki wa Simba waelewe hakuna mtu ambaye anapinga jitihada zilizofanywa na Mohammed Dewji , kila mtu anatambua mchango wake, Mjadala ambao tunajadili ni uhalali wa bodi ya Simba “

“Simba inatakiwa kuwa chini ya Mangungu lakini mashabiki hawataki kulisikia hilo , leo hii tunaambiwa Mo anarudi ! Je anakuja kuwa mwenyekiti wa bodi ipi ? “

“Ili bodi iwe hai ni lazima mchakato uwe umekamilika , huu mchakato wa Simba umekwama”

“Uongozi wa Simba uliopo ,upo kwa nguvu ya wanachama ambayo ndio Simba ya sasa hivi na kiongozi wao ni Mangungu na yeye ndio anayeendesha shughuli za kila siku za klabu”

“Mo kama anataka kuingia Simba na ili awe na nguvu kwa huu mfumo uliopo sasa hivi inabidi asubiri miaka minne ufanyike uchaguzi agombee kama Mangungu”

“Baada ya hapo atakuwa mwenyekiti wa Simba ambaye anatambulika kiutaratibu wa uendeshaji wa Klabu”

“Kinachofanyika sasa hivi ni kwa sababu Mo ana hela sana lakini lazima kuwe na utaratibu unaoeleweka na watu wasifiche vitu”
 
  • Like
Reactions: Amosi Simon

De hexane jr

Mgeni
Jun 10, 2024
4
1
5
Anatumiwa na watu huyooo
Kwakuwa watu tunamfuatilia ndo maana upande wa pili wanaamua kumtumia ili atuvuruge
kwanza kabisa tunajua kuwa @ShaffihDauda ni mwana utopolo lialia
Hivyo sisi tuliosoma Cuba tayari tunaelewa kuwa anatupoteza maboya na hiyo ramani ya mchongo anayotucholea kitaaaambo tunayo org.com yake🤣🤣
Mwambien @ShaffihDauda Tuna D tatu sio mbili tena.