Lewandowski Mchezaji Bora wa FIFA 2021.

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
407.jpg

MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Poland ambaye anakipiga Bayern Munich Robert Lewandowski ameshinda tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora wa mwaka 2021 wakati mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo akitwaa tuzo maalumu.
Lewandowski, 33, ametwaa tuzo hiyo ikiwa ni mara ya pili mfululizo ambapo katika kipindi hicho ametupia bao 69 akimshinda Lionel Messi na Mohamed Salah wa Liverpool.
Ronaldo ameshinda tuzo ya mfungaji bora wa muda wote kimataifa. Lewandowski moja ya washambuliaji hatari kwa hivi sasa duniani, alivunja rekodi ya Mjerumani Gerd Muller ya miaka 49, ambapo alifunga goli 43 katika mechi 34 za Ligi kwenye kipindi kimoja cha msimu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Robert Lewandowski:
"Messi na Cristiano walitengeneza historia nyingi pamoja na kushinda mataji yote iwezekanavyo.
Binafsi sipati picha namna ambavyo Mbappe na Haaland watatawala soka la dunia kama walivyofanya Leo Messi na Cristiano, wamefanya hivyo karibu miaka 12."
Chanzo: France Football

Inaweza kuwa picha ya Watu 2 na watu wanasimama