
MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Poland ambaye anakipiga Bayern Munich Robert Lewandowski ameshinda tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora wa mwaka 2021 wakati mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo akitwaa tuzo maalumu.
Lewandowski, 33, ametwaa tuzo hiyo ikiwa ni mara ya pili mfululizo ambapo katika kipindi hicho ametupia bao 69 akimshinda Lionel Messi na Mohamed Salah wa Liverpool.
Ronaldo ameshinda tuzo ya mfungaji bora wa muda wote kimataifa. Lewandowski moja ya washambuliaji hatari kwa hivi sasa duniani, alivunja rekodi ya Mjerumani Gerd Muller ya miaka 49, ambapo alifunga goli 43 katika mechi 34 za Ligi kwenye kipindi kimoja cha msimu.