Ligi Kuu Ya NBC Inarejea , Una Jambo Gani La Kuwashauri Waamuzi?

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
515
677
125
Ligi Kuu ya NBC ligi ya nne kwa ubora barani Afrika inarejea wikiendi hii febuari 1 baada ya mapumziko ya takribani mwezi mmoja .

Ligi hiyo itaanza kwa michezo miwili ya viporo vya mzunguko wa 16 ambavyo ni mechi za Yanga dhidi ya Kagera Sugar Februari 1 katika uwanja wa KMC mkoani Dar es Salaam.

Februari 2 Tabora United itakuwa mwenyeji wa Simba katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora katika mchezo uliokuwa umepangiwa tarehe mpya.

Mzunguko wa 17 utaanza rasmi februari tano hadi saba kwa michezo nane itakayochezwa katika viwanja mbalimbali nchini .
 

Frank Ngissa

Mpiga Chabo
Jan 31, 2025
1
0
0
Hakika tulikuwa tumeisubiri kwa hamu sana ligi kwa wakati ambapo ilikuwa imesimama.... hivyo ni mafikirio yangu kwamba iwapo waamuzi wakisimama katika haki na kufuata kanuni na sheria za mpira hakika ligi itakuwa Bora zaidi na tutafurahia burudani na madavidavi mengi sana katika soka.