Liverpool Thread

Mkwavinyika

Administrator
Staff member
Dec 2, 2021
49
9
26
Dar es Salaam
Mechi ya Liverpool inayofuata



Taarifa za Club

 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
WENYEJI, Liverpool usiku wa alhamisi wamewatandika Newcastle United mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield, Liverpool.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Diogo Jota dakika ya 21, Mohamed Salah dakika ya 25 na Trent Alexander-Arnold dakika ya 87 baada ya Newcastle kutangulia kwa bao la Jonjo Shelvey dakika ya saba.
Liverpool inafikisha pointi 40, lakini inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 17.
Hali inazidi kuwa mbaya kwa Newcastle United ikibaki na pointi zake 10, yaani inaizidi tu wastani wa mabao Norwich City inayoshika mkia.
 

Attachments

  • liverpool.PNG
    liverpool.PNG
    527.5 KB · Somwa: 0

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

SALAH AKOSA PENALTI, LIVERPOOL YAPIGWA 1-0​

1640758806662.png
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah jana alikosa penalti Liverpool ikichapwa bao 1-0 na wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa King Power.
Mkwaju wa penalti wa Salah ulipanguliwa na kipa Kasper Schmeichel dakika ya 15 na alipojaribu kuunganisha mpira uliorudi ukagonga mwamba.
Bao pekee la Leicester City lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Everton, Ademola Lookman dakika ya 59 na kwa ushindi huo katika mchezo wa 18 wanafikisha pointi 25 katika nafasi ya tisa.
Kwa upande wao Liverpool wanabaki na pointi zao 41 katika nafasi ya pili, sawa na Chelsea ya tatu, wote wakiwa nyuma ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya timu zote kucheza mechi 19.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA ENGLAND​

1642397447700.png
WENYEJI, Liverpool wamefufua matumaini ya ubingwa baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumapili Uwanja wa at Anfield.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Fabinho dakika ya 44, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 69 na Takumi Minamino dakika ya 77 na kwa ushindi huo kikosi cha Jurgen Klopp kinafikisha pointi 45 katika mchezo wa 21, kikizidiwa pointi 11 na mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Brentford yenyewe inabaki na pointi zake 23 za mechi 21 katika nafasi ya 14.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL YAITANDIKA CRYSTAL PALACE 3-1 SELHURST PARK.​

AVvXsEiXCRGkM9l4ngnwtoCjIj7umlraU_zmAsf80ljPNR2JhxWL5r8yeOCHWfJ3q0ntyweOhqMjeOQpe-7iNqyl6GxHuDz5kWDBjnoIjkCfGvHTTocH6ClAjrw4VKiiZDhpkrG-1SpjRp4EO1daQPo4VCVrc6ozx_0m1qK68mJ61OKAHRiu_lTdcI8KuU8r=w640-h378

TIMU ya Liverpool imewachapa wenyeji, Crystal Palace mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumapili Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Virgil van Dijk dakika ya 18, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 32 na Fabinho kwa penalti dakika ya 89, wakati la Crystal Palace limefungwa na Odsonne Edouard dakika ya 55.
Liverpool inafikisha pointi 48 katika mchezo wa 22, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tisa na Manchester City ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Crystal Palace inabaki na pointi zake 24 za mechi 22 katika nafasi ya 13.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
HAKUNA KUPUMZIKA
Mo Salah
🇪🇬
amerejea mazoezini akiwa na kikosi cha Liverpool mara baada ya kumaliza majukumu yake ya timu ya Taifa ya Egypt
🇪🇬
.
273495322_5085404091519500_929677793115149986_n.jpg
273522985_5085404094852833_2358303564590344264_n.jpg
273496538_5085404098186166_370772538548174451_n.jpg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Sadio Mane, Mo Salah Kufanya Kikao na Klopp.​

klopp-salah.jpg

Nahodha wa timu ya Misri, Mohammed Salah anataraji kujiunga na klabu yake ya Liverpool leo Februari 8, 2022 na kuna uwezekano mkubwa wa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kwenye mchezo wa EPL dhidi ya Leicester City Alhamis ya Februari 10, 2022.
Kwa Upande mwingiine, Nahodha wa Senegal, Sadio Mane ambaye ametwaa ubingwa wa AFCON naye anatarajiwa kurejea klabuni hapo Jumatano au ya Alhamis wiki hii kukutana na mshambuliaji mwenzake Mohammed Salah ambaye alicheza walikuwa wapinzani kwenye fainali ya AFCON Februari 7, 2022 Nchini Cameroon.
Naye Kocha mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp aliweka wazi kuwa ataongea na wachezaji hao pindi watakaporejea baada ya kumalizika michuano ya AFCON ili kuwasahaulisha yaliyojiri katika kombe la mataifa ya Africa walipokua wapinznai hasa kwenye mchezo wa fainali ambapo Mohammed Salah alionekana kuumia sanaa baada ya kukosa ubingwa huo.
Kipindi ambacho Mane na Salah walikua kwenye majukumu ya timu zao za taifa katika michuano ya AFCON, Liverpool ilicheza michezo sita kwenye michuano yote na wameshinda michezo yote ikiwemo michezo miwili ya ligi kuu ya England na pamoja na michezo miwili ya nusu fainali ya kombe la carabao dhidi ya Arsenal.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

JOTA APIGA ZOTE MBILI LIVERPOOL YAILAZA LEICESTER 2-0.​

AVvXsEjjG_W8wvx93IgU2KM9-ER_mhp1scO4tfvzZRLLrTF7RlN7VWHwwD9hd0NLsD4SwejVBaQduknqx4vYapl3zQK7iehhAaCwwjWzvA8bC1c4vplNPCUYj78QweVsOxlIcu5nKmG0jbfHOk0_j7GHveNZWBhBEez2N5DhVNIjiQiNBC4Q4LFrnDKFlGic=w640-h426

MABAO ya Mreno, Diogo Jota dakika ya 34 na 87 yameipa Liverpool ushindi wa 2-0 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Anfield.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 51 katika mechi ya 23, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tisa na mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Leicester City inabaki na pointi zake 26 za mechi 21 sasa katika nafasi ya 12.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL YAICHAPA BURNLEY 1-0 TURF MOOR.​

AVvXsEgCQFwfiSxBmEYt3jZ0Xu_VaHsbuYMOuPhzdBgYfEV2Nap7t56pgHeKKbKZdd5PvA2z2wm1-EN8mJhNTA9JegX5mJ_R8fAH5YBeOlfpwwlwZLR9enCtxuMx-neziT6OpCsDqOF8I_O_2F0is44L9JIVneijql4vrvjaFUK4x2xYiPy40mFJvMSrjnU3=w640-h420

BAO la Fabinho dakika ya 40 limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Turf Moor.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 24, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tisa na mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Hali inazidi kuwa mbaya kwa Burnley ambayo inaendelea kushika ikiwa na pointi 14 baada ya kucheza mechi ya 21 leo.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Klopp Amsifu Mo Salah Kwa Mabao 150
P2020-09-12-Liverpool_Leeds-122.jpg

JURGEN Klopp amekiri kuwa hakuna aliyetarajia kuwa Mo Salah atakuwa gwiji wa kufunga mabao Liverpool haraka namna hiyo kufuatia Mmisri huyo kufunga bao lake la 150 juzi kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Norwich.
Salah alionekana atakuwa wa kawaida tu aliposajiliwa na Liverpool kutokea Roma kwa pauni mil 36 mwaka 2017 kutokana na kucheza kawaida alipokuwa na Chelsea hapo awali.
Hata hivyo, alifunga katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Watford na tangu hapo hajaacha kufunga. Sasa amefikisha mabao 150 katika mechi 233, na ameweka rekodi ya kuwa na uwiano bora zaidi wa mabao ukilinganisha na mechi alizocheza, kuliko mchezaji yeyote wa Liverpool kihistoria ambaye ameifungia klabu hiyo mabao zaidi ya 30.
Hii maana yake ni kwamba amefikisha idadi ya mabao 150 kwa haraka zaidi, yaani katika mechi chache zaidi.
“Bao lake la kwanza pale Watford pengine ndilo lilikuwa rahisi zaidi. Alifunga mabao mengine 149 ndani ya kipindi kifupi sana,” alisema Klopp.
“Siwezi kukumbuka mabao yake yote lakini nayakumbuka mengi na kulikuwa na mabao mengine mazuri zaidi. Dhidi ya Chelsea, akifunga kutoka kwenye kona, alipofunga baada ya kukokota mpira dhidi ya Manchester City, dhidi ya United kwa pasi ya Alisson. Na leo (juzi) lilikuwa bao zuri kusema ukweli.”
Salah sasa amekuwa mmoja wa wachezaji 10 tu katika histori
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL YAISHINDILIA LEEDS 6-0 ANFIELD​

AVvXsEgpLruB8wXh7medzUarf-WGNZHij3PXeZR9xge1TERX8Opgdhm4U1WaNKcwgobDZbb2rIwsqiyBESg3DCaXpNbyvRZXP1jM17E7dRt8fS1UyViSfry2OqaRcwrYdC-X30XZ-e5rNIL_VUXWAoguyAa0jvZ1fYFJ1QBATBpZOhY_OlT1q74UTPC79F5G=w640-h436

WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa 6-0 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield usiku wa Jumatano.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mohammed Salah kwa penalti yote mawili, dakika ya 15 na 35, Joel Matip dakika ya 30, Sadio Mane mawili pia dakika ya 80 na 90 na beki Virgil Van Dijk dakika ya 90 na ushei.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 60, sasa ikizidiwa tatu tu na Mabingwa watetezi, Manchester City baada ya timu zote kucheza mechi 26, wakati Leeds inabaki na pointi zake 23 za mechi 25 nafasi ya 15.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL WATWAA CARABAO KWA MATUTA​

AVvXsEi1zbzmZ0qOMhNW7STOeZXgSFM2IVEa9P5GqquDnH6cAA_9sRPT8KnObc9sTin3foU6HgL0lnEhXVVSHKAGQlO52bVQ6zeqSIUhGXz3yryHLrUxKH90VTi4uYmRZ18s0eDc_elzs5euUckQXTltXO6Ks0gGM73De5yWDrH3cEzehsTyjkjmMA_nzQU-=w640-h352


TIMU ya Liverpool imefanikiwa kutwaa Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa penalti 11-10 kufuatia sare ya 0-0 na Chelsea usiku huu Uwanja wa Wembley Jijini London.
Kipa Kepa Arrizabalaga aliyeingia dakika ya 119 maalum kwenda kuokoa mikwaju ya penalti, hakuweza kuokoa hata moja na bahati mbaya zaidi kwake akaenda kupiga juu ya lango penalti yake ya mwisho.
Waliofunga penalti za Liverpool ni Jamaa Milner, Fabinho, Virgil van Dijk, Trent Alexander-Arnold, Mohamed Salah, Diogo Jota, Divock Origi, Andrew Robertson, Harvey Elliott, Ibrahima Konaté na kipa Caoimhin Kelleher.
Waliofunga penalti za Chelsea ni Marcos Alonso, Romelu Lukaku, Kai Havertz, Jorginho, Antonio Rüdiger, N'Golo Kanté, Timo Werner, Thiago Silva na Trevoh Chalobah.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Kwa mujibu wa Telegraph, Mlinzi wa kati wa klabu ya Liverpool Virgil van Dijk alitoa mchango wa kiasi kikubwa cha fedha kwa timu ya Taifa ya viziwi ya Uholanzi baada ya kujua matatizo yao ya kifedha yanaweza kuwazuia kushiriki mashindano ya Deaflympics nchini Brazil mwezi Mei.
What a Man
🔥

Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na amesimama
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

MANE AIFUNGIA BAO PEKEE LIVERPOOL YASHINDA 1-0

BAO pekee la mshambuliaji Msenegal, Sadio Mane dakika ya 27, limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfield.
Liverpool inafikisha pointi 63, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu tu na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya kila timu kucheza mechi 27.
West Ham United baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi 45 za mechi 28 nafasi ya tano.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah pamoja na wakala wake hawana nia ya kukubali ofa ya sasa ya mkataba mpya wa Liverpool
🔴

Imeelezwa kuwa Kipaumbele cha Salah kwasasa ni kusalia Liverpool lakini hana nia ya kukubali pendekezo lililopo mezani la kuongeza mkataba.
Liverpool kazi kwenu, Fundi wa Mpira anataka pesa
💵

Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Mlinzi wa kati wa Liverpool Joel Matip ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya England
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1


 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

LIVEROOOL YAICHAPA BRIGHTON 2-0 UGENINI​


TIMU ya Liverpool jana imepata ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa The AMEX.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Luis Diaz dakika ya 19 na Mohamed Salah kwa penalti dakika ya 61 baada ya Yves Bissouma kuunawa mpira.
Kwa ushindi huo Liverpool inafikisha pointi 66, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tatu na Manchester City wanaoongoza, wakati Brighton inabaki na pointi zake 33 katika nafasi ya nane baada ya timu kucheza mechi 28.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

LIVERPOOL YAICHAPA WATFORD 2-0 ANFIELD​


TIMU ya Liverpool jana iliichapa Watford mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anflied.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya 22 na Fabinho dakika ya 89 kwa penalti na kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 72, ingawa inabaki na nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 30.