LIVERPOOL YAITANDIKA MAN UNITED 4-0 ANFIELD
WENYEJI, Liverpool wamewatandika mahasimu, Manchester United mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa Anfield.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Luis Diaz dakika ya tano, Mohamed Salah mawili, dakika ya 22 na 85 na Sadio Mane dakika ya 68.
Liverpool inafikisha pointi 76 katika mchezo wa 32 na kupanda kileleni, ikiizidi pointi mbili Manchester City ambayo ina mechi moja mkononi na leo inacheza na Brighton & Hove Albion, wakati Man United inabaki na pointi zake 54 za mechi 33 sasa nafasi ya sita.