Haya mimi nimeyaita maajab maana haijawahi kutokea na huenda wengine hili hawakuliona.
Jana YANGA walipokuwa wanacheza mchezo wa kirafiki na AUGSBURG ya Ujerumani, nilimuona Chota Chama akifanyiwa substitution (mabadiliko) ktk kipindi cha pili. Maajabu kwangu ni pale Chama alipoitwa kutoka akatoka kiroho safi tena huku AKIKIMBIA. Kitendo hiki kiliniacha na mshangao maana haikuwahi kutokea pindi yupo SIMBA.
Wakati yupo SIMBA alipokuwa akifanyiwa substitution alikuwa anatoka kwa kununa na wakati mwingine alikuwa anatoka na kuzira kabisa hakai kwenye benchi badala yake anaenda kupumzika chumba cha kubadilisha nguo.
Je kwa tukio la jana CHAMA alituma ujumbe gani kwa timu ya SIMBA na mashaabiki wake? Ama kweli bora umfadhili mbuzi utakunywa supu lakini siyo mwanadamu. Nilwaza sn kwamba hivi ndiyo huyu mashaabiki wa SIMBA walimhusudu na kumtukuza kwa jina la Mwamba wa Lusaka!!! Mara mzee wa local motive.
NB
Ushauri wangu kwa SIMBA na YANGA acheni kupaparikia wachezaji na kuwapa UFALUME ambao hata wewe nyumbani kwako hauna. Mnawasifia wachezaji kiasi cha kuwafanya nao kujihisi bila wao timu haiwezi kusonga mbele. Wakati mwingine hasa hawa wachezaji wa kigeni wamekuwa wanasifiwa na kutukuzwa na mashaabiki na vyombo vya habari hadi kuwafanya kujiona km nao sasa ni raia wa Tanzania.
Km siyo ushamba basi punguzeni mihemko kwa hawa wachezaji wa kigeni. Mbona wachezaji wa ndani hamuwapi huo UFALUME. Ebu angalia kazi anayofanya JOB, BAKA, na nk pale YANGA. Pale SIMBA yupo ZIMBWE (SHABALALA) KAPOMBE, MANULA nk. Hawa wote wamezitumikia timu zao kwa uadilifu mkubwa sn na muda mrefu tena kwa mshahara wa kawaida sana lakini hawaimbwi na mashaabiki wala vyombo vya habari zaidi ya kuwaponda pindi siku hawapo mchezoni. Utaskia wanasifiwa akina DIARA, PAKOME, CHAMA, YAOYAO,, AZIZI KEY, LAKRED MALOME tena huyu wamempa eti jina la UKUTA WA YERIKO. Mbona hayo majina hatuayasikii kwa wazawa.