MAPINDUZI CUP 2022.

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Yanga rasmi imevuliwa ubingwa wa Mapinduzi na Azam FC baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 9-8 baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana mechi ya nusu fainali.
1641876135810.png
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

NI SIMBA NA AZAM FAINALI MAPINDUZI ALHAMISI.​

1641877378834.png
MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Namungo FC usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 15 na winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 50 na sasa watakutana na Azam FC waliowatoa mabingwa watetezi, Yanga SC kwa penalti 9-8 kufuatia sare ya 0-0 leo hapo hapo Amaan. Fainali itachezwa Alhamisi Saa 2:15 usiku.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Azam safari hii haitaki matuta, yapiga kikao kizito​

1642059244927.png
UNGUJA. Bosi wa Azam FC ambaye ni Afisa Mtendaji mkuu Abdulkarim Amin 'Popat' amewataka wachezaji wake kumaliza mechi ya fainali na Simba mapema bila kusubiri kupigiana penalti.

Azam kesho Alhamisi Januari 13 inawakaribisha Simba katika fainali za Kombe la Mapinduzi zitakazofanyika kuanzia saa 2:15 usiku kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani hapa.

Popat amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu kwa pande zote mbili lakini amekaa na wachezaji wao pamoja na benchi la ufundi kuona namna gani watamaliza mechi hiyo bila kufika hatua ya penalti kama ilivyokuwa mechi yao ya nusu fainali dhidi ya Yanga huku wao wakisonga mbele kwa matuta 9-8.

Amesema kuwa kama viongozi wamemaliza kazi yao kilichobaki ni upande wa benchi la ufundi kuona nani atafaa kesho avae jezi kuwania ubingwa wenye thamani ya Sh 25 milioni huku wachezaji nao wakipewa jukumu la kupambana uwanjani.

"Sitaki hata kusikia mambo ya penalti hata zile zilizopigwa na kupigiwa wakati wa nusu fainali sikuiona hata moja ikipigwa nilikuwa naangalia chini hivyo tumekaa nao na kuwaambia fainali tusifike kwenye matuta naamini tutaimaliza mechi mapema tu kwenye muda wa dakika 90," amesema Popat

Mshindi wa pili atajinyakulia Sh 20 milioni kutoka kwa waandaaji wa Kombe la Mapinduzi na hii ni mara yao ya tatu kwa timu hizo kukutana fainali, mara mbili Azam imemfunga Simba.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Alikiba kutumbuiza Fainali Mapinduzi Cup.​

1642059395322.png

UNGUJA.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Alikiba kesho Alhamisi anatarajiwa kutumbuiza kwenye fainali za Kombe la Mapinduzi zitakazoanza saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan kisiwani hapa.

Fainali hiyo inazikutanisha Azam FC na Simba baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali ambapo Azam iliitoa Yanga kwa penalti 9-8 wakati Simba iliifunga Namungo FC bao 2-0.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindani hayo Imane Osmond Duwe kuwa mbali na Alikiba pia kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka vikundi vya sanaa kisiwani hapa.

"Kutakuwa na burudani mbalimbali kwenye fainali hizo hizo lakini kubwa ni Alikiba msanii mkubwa kutoka Bara. Ni fainali za aina yake msimu huu na yamekuwa na ushindani mkubwa tangu yalipoanza," amesema Imane.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba kucheza fainali mbele ya Rais Mwinyi.​

1642059523391.png
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye fainali za Kombe la Mapinduzi itakayozikutanisha Azam na Simba kesho kuanzia saa 2.15 usiku kwenye Uwanja wa Amaan.
Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano hayo Imane Osmond Duwe amesema kuwa kutokana na ukubwa na umuhimu wa mashindano hayo Rais ndiye atakayeyafunga.
Amesema kuwa utaratibu mzima kesho utabadilika ambapo Rais huyo atakuja na wageni wake kushuhudia fainali hiyo ambayo inazikutanisha timu hizo ikiwa zinakutana kwa mara ya tatu huku mara mbili Simba ikifungwa na Azam FC.
Moja ya mabadiliko hayo ni katika uuzwaji wa tiketi za mechi ambapo sasa kutakuwa na tiketi 50 pekee za VVIP huku zingine zitabaki kuwa Sh 3000, 5000 na 10000.
"Hao 50 ndiyo watakaoingia kupitia pale VIP lakini wengine wote watapewa utaratibu maalumu wa kuingia ila tunawaomba mashabiki wafike mapema kuepuka msongamano.
"Rais wetu Hussein Mwinyi ndiye atatufungia mashindano hayo ambapo atakuwa na wageni wake wa kiserikali wakiwemo makamu wake. Viingilio vilivyobadilika ni tiketi za VVIP ambazo ni maalumu kwa baadhi ya watu," amesema Imane
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI 2022​

1642138087809.png
BAO la penalti la mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddi Kagere limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC katika Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kagere alifunga bao hilo dakika ya 56 baada ya winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho kugongana na kipa Mganda wa Azam FC, Mathias Kigonya na hilo linakuwa taji la nne la Mapinduzi kwa Simba baada ya awali kulibeba mwaka 2008, 2011 na 2015.
Baada ya mchezo, beki Mkongo, Hennock Inonga Baka ‘Varane’ alichaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi, wakati winga Sakho alichaguliwa Mchezaji Bora wa Mashindano, Aishi Manula Kipa Bora na Kagere Mfungaji Bora huku chipukizi Tepsi Evance wa Azam FC alipewa Tuzo ya Mchezo wa Kiungwana.
Aishi, Baka, Kagere na Sakho kila mmoja alipewa Sh. Milioni 2, wakati Tepsi alipewa Sh. 300,000.

1642138184651.png
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi alimkabidhi Nahodha wa Simba Kombe na mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 25, wakati Azam FC walipewa Sh. Milioni 15.

1642138275631.png
1642138319408.png
1642138356884.png