Hii mechi mbungi ilipigwa, jasho na damu viliwatoka wachezaji waliokua nabkiu ya kumkatisha tamaa Messi na Wengine wakiwa na Shauku ya kumuona Messi akifanikiwa. Mwisho wa siku wakajikuta wanatupa burudani yenye vitimbwi ndani yake haswaaa.
Kwako wewe, ipi ilikuwa bora kuzidi hii?
Mechi ya fainali kwangu ni bora sana, maana ilifika wakati tunaona bingwa ni ARGENTINA, lakini dakika chache kabla mechi kuisha, tukaanza kujiuliza kombe linaenda wapi? Maana ilikuwa piga nikupige, na vuta nikuvute.
Kitu kingine cha kipekee kabisa kwangu ni namna referee Szymon Marciniak kutoka Poland alivyochezesha mchezo kwa weledi sana, na alifanya mchezo wa soka uwe na ladha yake ya asili kwakuwa hatukuwa na VAR check hata moja, japokuwa kulikuwa na matukio yenye utata, lakini referee Szymon Marciniak hakutetereka na maamuzi yake hata mara moja, na alikuwa fair.